Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge asema wanaume wakubali hawana nguvu za kiume, naibu waziri amjibu

92500 Mbunge+pic Mbunge asema wanaume wakubali hawana nguvu za kiume, naibu waziri amjibu

Tue, 21 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) nchini Tanzania, Susan Lyimo ameishauri Serikali ya nchi hiyo kutoa elimu ya sababu ya wanaume kutokuwa na mbegu zenye nguvu ili kunusuru ndoa.

Susan ametoa ushauri huo wakati kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii ilipokuwa ikipokea taarifa ya utekelezaji wa shughuli zake jana Jumatatu Januari 20, 2020.

“Kwa kweli ndoa nyingi sana zinavunjika. Na ndoa hizi zinavunjika kwa sababu ya watu kutopata watoto, tatizo hili lilikuwapo lakini linaongezeka,” alisema Lyimo.

Alisema kwa sababu ya mfumo dume walikuwa wanasema mwanamke ndiye mwenye tatizo lakini sasa hivi tatizo hilo limegeuka kwa wanaume.

“Wanaume nao wakubali kwa sababu nao wana tatizo. Mimi nilikuwa nadhani kuna haja ya kutoa elimu tuone nini sababu za wanaume kutokuwa na mbegu zisizokuwa na nguvu ili wake zao ama wanawake zao wapate watoto,” amesema.

Amesema kama wakienda kupima vinasaba watakuta watoto wengi sana baba zao sio kwa sababu baada ya mwanamke kuambiwa kuwa hazai anaamua kuchepuka ili apate mtoto.

Pia Soma

Advertisement
“Kuna haja ya kutoa elimu ili kuhakikisha tunanusuru hizi ndoa kwa sababu. Mimi kama mshauri naletewa matatizo makubwa zaidi. Wanajinusuru kuogopa kupewa talaka,” alisema ambaye ni waziri kivuli wa elimu, sayansi na teknolojia

Akijibu hoja hiyo, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii , Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndungulile alisema changamoto ni kubwa sana na kwamba Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Dar es Salaam imeanza maandalizi ya kutoka huduma ya ugumba.

“Tafiti duniani zinaonyesha kuwa kwa miaka 50 kumekuwa na punguzo la asilimia 50 ya nguvu za kiume. Nilikuwa nasoma tafiti moja inasema katika miaka 50 ijayo basi wanaume wote hapa tutakuwa hamna kitu,” alisema.

Alitaja visababishi kuwa ni pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa, aina ya maisha na vyakula.

Hata hivyo, Dk Ndungulile alisema si kweli watoto wengi wanabambikiwa baba kwa sababu wanaokwenda kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ni wale wenye hofu vya kuwa watoto si wao.

Alisema hata wale wenye hofu na kwenda kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kupima ni chini asilimia 50 ndio wanagundua kuwa wamebambikiziwa watoto.

Chanzo: mwananchi.co.tz