Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge asema wananchi wanahangaika kupata huduma ya afya usiku, Serikali yamjibu

Fri, 21 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mbunge wa Kibiti (CCM) Ally Ungano ameiomba Serikali ya Tanzania kupeleka taa maalum katika zahanati na vituo vya afya jimboni kwake ili kuwasaidia wagonjwa na wanawake wanaopata tiba nyakati za usiku.

Ungano ametoa kauli hiyo Bungeni leo Ijumaa Juni 21,2019 alipouliza swali la nyongeza kufuatia jibu la Serikali katika swali lake lililohoji Serikali ina mkakati gani kupeleka umeme kwenye visiwa hivyo na watapeleka umeme wa aina gani.

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amesema vijiji vilivyopo katika Delta ya mto Rufiji vya Pombwe, Kiongoroni, Mbuchi, Mbwera, Maporoni, Kiechuru, Msala, Kiasi, Kiomboni, Mchinga na Msifuni vimeshafanyiwa upembuzi yakinifu kwa ajili ya kupelekewa umeme.

Amesema baada ya upembuzi kufanyika, baadhi ya vijiji vikiwemo Mbuchi, Mbwera Mashariki na Magharibi vitaunganishwa umeme wa gridi ya taifa kutoka Muhoro umbali wa kilomita 40.

Hata hivyo, Naibu Waziri amekubali kuwa ni muhimu kuwapelekea taa maalum katika maeneo hayo kwa kuwa kuna matatizo.

Chanzo: mwananchi.co.tz