Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge aihoji serikali wananchi kujipima VVU wenyewe

15923 Vvu+pic TanzaniaWeb

Thu, 6 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Suzan Lyimo ameihoji Serikali ni lini itatoa nafasi kwa watu kujipima wenyewe maambukizi ya virusi vya Ukimwi kwani baadhi wanataka kufanya ngono za chapchap.

Lyimo ameuliza swali hilo leo bungeni Septemba 6, 2018 na amesema watu wanakosa nafasi hiyo kutokana na kutokuwa na ruhusa hiyo.

"Kuna watu wanataka kujua afya zao kwani wanataka kufanya ngono za chapchap, lakini majira ya usiku vituo vya afya vinakuwa vimefungwa. Je, Serikali haioni umuhimu wa kuruhusu kujipima?" amehoji Lyimo.

Akijibu swali hilo, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema mpango huo ni mgumu katika utekelezaji kwani wengi wakijipima wanaweza kuwa na msongo wa mawazo na kusababisha kuambukiza wengi.

Hata hivyo, Mwalimu amesema Serikali imeanza mchakato wa kuwa na sheria ya kuruhusu watu kujipima lakini kwa sharti la kuwa mbele ya mtaalamu siyo peke yao.

Katika swali la msingi, Hawa Mchafu (Viti Maalum CCM) ametaka kujua mkakati wa Serikali wa kumaliza kabisa ugonjwa wa Ukimwi nchini.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge) Antony Mavunde amesema iko mikakati mbalimbali ya kuhakikisha Ukimwi unatokomezwa ifikapo 2030.

Ametaja baadhi ya mikakati hiyo ni kuhamasisha makundi ya kijamii kuendelea kupima afya zao na kuchukua tahadhari ikiwamo matumizi ya ARVs.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz