Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbeya yaboresha matibabu ya viungo

Viungo Viungoooo.png Mbeya yaboresha matibabu ya viungo

Fri, 20 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya imezindua jengo jipya la kutolea huduma ya tiba mazoezi (Fiziotherapia), kwa ajili ya kupanua wigo wa upatikanaji wa huduma kwa wagonjwa wenye matatizo ya maumivu ya viungo.

Awali Hospitali hiyo lilikuwa na uwezo kuhudumia wagonjwa wa nje 30 hadi 40 kwa siku lakini baada ya uzinduzi wa jengo hilo sasa itakuwa na uwezo wa kuhudumia wagonjwa wa nje kati ya 120 hadi 200 kwa siku.

Hayo yamebainishwa leo Okotba 19, 2023 wakati wa hafla hiyo ya ufunguzi wa jengo hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo Dk Godlove Mbwanji, ameushukuru uongozi wa hospitali pamoja kamati yote iliyofanikisha kukamilika kwa jengo hilo.

“Na mimi naomba shukrani zote nilizopewa ni za uongozi wa hospitali na watumishi wote kwa sababu vyote vilivyofanyika ni watumishi wamefanya kazi kupitia sehemu ya mapato yanayopatikana.” Dk Mbwanji

Pia ametoa rai kwa watumishi wa idara hiyo inayohusika na huduma ya tiba mazoezi kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kufanya mazoezi ili kuepukana na magonjwa yasiyo ya lazima.

Awali, mkuu wa idara ya fiziotherapia hospitalini hapo, Seraphine Mushi amemepongeza maboresho mbalimbali yaliyofanyika katika idara hiyo ikiwemo ongezeko la vifaa tiba pamoja na upanuzi wa jengo hilo.

“Hapo awali jengo hili lilikuwa na vyumba 16 vya matibabu na sasa vimeongezeka vyumba nane pamoja na eneo la kufanyia mazoezi ambavyo vitapelekea uwezo wa kutibu wagongwa wa nje 120 hadi 200 kwa siku ukilinganisha na zamani tulikuwa tukiona wagonjwa 30 hadi 40 kwa siku,” amesema Seraphine Mushi

Mathias Mkoma ni mmoja wa wagonjwa wanaopatiwa huduma ya matibabu kwa njia ya tiba mazoezi Hospitali hapo wamepongeza uongozi wa hospitali pamoja na watumishi wa idara hiyo kutokana na huduma wanazopatiwa.

“Tumefurahishwana huduma zinazopatikana katika idara hii hivyo hatuna budi kuupongeza uongozi wa hospitali, wahudumu wote pamoja na madaktari kwa kweli wanafanya kazi kwa upendo” amesema

Katika tukio hilo pia watumishi kutoka idara ya Fiziotherapia walipata nafasi ya kumkabidhi cheti Dk Mbwanji kama ishara ya kutambua mchango wake kutokana na ushirikiano anao uonyesha katika jitihada za kuboresha huduma hospitalini hapo

Chanzo: www.tanzaniaweb.live