Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mazoezi mepesi ni mtaji wako kiuchumi zaidi

23499 Mazoez+pic TanzaniaWeb

Mon, 22 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Katika kutafuta maisha kwenye nchi zinazoendelea ambazo zinazopambana kwenda katika uchumi wa kati bado mazoezi yanasahaulika kama ni moja ya mtaji mzuri kiuchumi.

Ufanyaji wa mazoezi unaweza kuwa ni mtaji wa kiuchumi kwasababu yanakuepusha na magonjwa yasiyoambukiza ikiwamo magonjwa ya moyo, figo, kiharusi na kisukari ambayo yanagharimu fedha nyingi katika uchunguzi na matibabu.

Ili kuyafanya mazoezi haya kuwa mtaji wa kiuchumi unahitaji kushikamana na mazoezi mepesi wakati wote wa maisha yetu ya kila siku.

Hulka ya kupenda mazoezi hutakiwa kujengwa mapema katika umri mdogo ili angalau ifike mahali ukikosa mazoezi haya ujione mkosaji unayepoteza mtaji wa maendeleo.

Mazoezi haya kitaalam hujulikana kama Aerobic exercises ambayo ni kama vile kutembea, kukimbia, kuruka kamba, kuendesha baiskeli, kuogelea, kucheza mziki na ufanyakazi zinazojongesha mwili.

Mazoezi hayana gharama kwani huitaji kulipia pesa kuyafanya katika kituo maalum bali tu unahitaji muda wa nusu saa tu kwa siku kwa siku tano za wiki.

Hata Rais wa Jamhuri ya muungano John Pombe Magufuli na Mke wake Janet Magufuli wanafanya mazoezi mepesi katika fukwe za feri zilizo jirani na ikulu ambazo huitaji kulipia chochote.

Mazoezi yanawafanya watu kuishi miaka mingi, kutozeeka, kuonekana wang’aavu na miili imara yenye kuweza kukabiliana na magonjwa.

Rais mstaafu wa awamu ya pili Ally Hassan Mwinyi mwenye umri wa miaka 94 mazoezi ni sehemu ya maisha yake na yamempa matokeo chanya kimaisha ikiwamo kuishi miaka mingi na kufikia umri huo.

Mazoezi haya yanachangia ngozi kuwa na afya njema hivyo kukupunguza gharama za kufanya huduma za ngozi saluni na matumizi ya vipodozi vyenye gharama kubwa.

Haijalishi una hadhi gani kufanya mazoezi ni moja ya mipango ambayo unatakiwa kuiweka katika ratiba za siku za kila siku, mara baada ya kazi au kabla.

Ndiyo maana watu wengi ambao wamepiga hatua kimaisha au wanaishi katika nchi zilizoendelea mazoezi huwa ni sehemu ya ratiba zao za siku.

Pamoja na kitendo kibaya cha kutekwa na watu wasiojulikana na kutoonekana mpaka sasa tajiri kijana Afrika Mohmed Dewji aliwahi kueleza ratiba yake ya siku ametenga muda wa kufanya mazoezi.

Hata tukio lilomkuta alikuwa akielekea kutimiza sehemu ya ratiba yake ya kufanya mazoezi, hii inadhihirisha kuwa mazoezi ni moja ya vitu muhimu kwa mtu anayetafuta mafanikio ya kimaisha.

Mazoezi huondoa hali ya uvivu na uchovu wa mwili, badala ya kukaa tu na kutazama luninga au kulala tu kunapofanya mazoezi yanakufanya kuwa na utimilifu wa mwili.

Mwili wenye mazoezi unakuwa si mvivu na anakuwa na mwamko wa kufanya kazi kwa bidii bila kuchoka hivyo kuweza kujitafutia maendeleo.

Mazoezi haya yanaokoa pesa nyingi kwani yanakuepusha na vishawishi vingi ikiwamo unywaji wa pombe au vilevi na anasa zisizo na ulazima.

Siku zote, hakuna kitu cha msingi kama mazoezi mepesi, yanasaidia kukufanya imara zaidi.

Chanzo: mwananchi.co.tz