Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Matumizi ya chanjo ya J&J yamefikia 80% Tanzania

CVGFDFGTRTD Zoezi la chanjo ya Corona limefikia asilimia 80 nchini

Mon, 4 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema zoezi la chanjo ya Uviko-19 limefikia zaidi ya asilimia 80 na zilizobakia mikoani hivi sasa ni chache.

Jumla ya chanjo milioni 1.058 zilizopokelewa nchini kutoka nchini Marekani Julai 24, 2021 na uchanjaji ulizinduliwa rasmi Julai 29, 2021 na Rais Samia Suluhu Hassan.

Kauli hiyo imekuja baada ya Serikali kuanzisha kampeni maalum ya kuhamasisha uchanjaji wa chanjo hiyo katika maeneo mbalimbali ikiwemo makanisani na kwenye mikusanyiko ya watu.

Majaliwa ameyasema hayo leo Jumatatu Oktoba 4 2021, wakati akifungua kongamano la tano la uwezeshaji lililoandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (Neec).

“Tunalo zoezi la uchanjaji. Namshukuru Mungu tumefikia asilimia 80 na kitu huko, tumebaki na chanjo chache sana kwenye mikoa hiyo. Kila mmoja awahi huko na kama kuna mahitaji tutaleta nyingine malengo ni afya,”amesema.

Amesema suala la chanjo sio lazima lakini ni muhimu kwaasababu linasaidia kuongeza virutubisho mwilini na iwapo mtu atapata hawezi kuwa mwepesi kama vile mtu ambaye hajachanjwa kabisa.

Amewaagiza wakuu wa mikoa kutoa elimu na kuhamasisha kuhusu umuhimu wa kuchanja chanjo hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live