Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Matumizi ya Shisha ni janga jipya nchini

Shisha Ban In Kenya Uvutaji shisha

Wed, 10 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) imesema ongezeko la wimbi la watumiaji wa Shisha umesababisha madhara makubwa kwa jamii, baada ya baadhi watumiaji kuanza kutumia kifaa hicho kuchanganyia dawa haramu za kulevya tofauti na matumizi rasmi ya kifaa hicho.

Kwa mujibu wa DCEA kifaa cha Shisha ni halali kwa matumizi ya tumbaku lakini baadhi ya watumiaji wamekuwa wakitumia Shisha kuvutia dawa haramu za kulevya.

Kamishna Msaidizi Kitengo cha Kinga na Huduma za Jamii wa DCEA, Moza Makumbuli amefafanua kuwa matumizi ya Shisha kwenye tumbaku yanaruhusiwa kisheria na unaweza kugundua endapo kifaa hicho kitatoa mvuke badala ya Moshi.

Hata hivyo matumizi ya Shisha ni hatari zaidi kwa afya kwani kwa mujibu wa tafiti ni kuwa unapovuta Shisha kwa muda wa saa moja ni sawa na kuvuta wastani wa sigara 100 hadi 200.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live