Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Matumizi holela tiba asili hatari kwa afya

12574d48abf361b71a7e1d2fd51444ed Matumizi holela tiba asili hatari kwa afya

Wed, 10 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MKURUGENZI Msaidizi wa Tiba za Asili kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Paul Mhame ametaka kuwepo na matumizi sahihi ya tiba za asili kwa kuwa ikitumika halela ni hatari kwa afya.

Alisema hayo jana jijini Dodoma ukiwa ni muendelezo wa kuelimisha jamii kujikinga na magonjwa yaliyo ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza.

“Watu wanakunywa kiholela aina tofauti tofauti za madawa, wengine wanatumia tangawizi kilo nzima, vitunguu saumu nusu kilo na malimao 20, hii ni hatari kwani ni rahisi kupata vidonda vya tumbo na ugonjwa wa koo, hivi vitu lazima vitumike kwa utaratibu,” alisema Dk Mhame.

Alisema hivi sasa kuna matumizi holela ya dawa na kwamba, wananchi wanazinunua na kuzitumia bila kuzingatia utaratibu.

“Watumie aina ya dawa na wafuate maelekezo sahihi na ikipita masaa 48 kama hujapata nafuu kutokana na dawa uliyoitumia nenda kituo cha afya,” alisema Dk Mhame.

Mkurugenzi wa Idara ya Tiba Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Dk Renald Subi alisema wanaendelea kuelimisha wananchi ili Tanzania ibaki salama.

Alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi inayozingatia maelekezo yanayotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO), kuhusu kujikinga na magonjwa na pia wanazingatia umuhimu wa tiba za asili.

Aliwataka Watanzania kuchukua hatua na tahadhari kuhusu kujikinga na virusi corona na kujiepusha na taarifa zisizo rasmi.

Aliwataka waganga wakuu wa mikoa na wilaya watumie miongozo iliyotolewa na wizara ya afya kuhusu kujikinga na ugonjwa wa COVID- 19.

Mkurugenzi Msaidizi wa Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza, Dk James Charles alisema jambo la muhimu ni kufanya mazoezi na kupata lishe bora.

Chanzo: www.habarileo.co.tz