Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Matokeo ya sensa yaonesha kuimarika uchumi wa wanawake

Mama Anne Makinda Matokeo ya sensa yaonesha kuimarika uchumi wa wanawake

Mon, 22 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Matokeo ya sensa ya watu na makazi yanaonesha viashiria vya kuimarika kwa hali za kiuchumi za wanawake katika kipindi cha miaka kumi ijayo.

Hayo yamesemwa na Kamisaa wa sensa ya watu na makazi Anne Makinda wakati wa mafunzo ya matumizi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi kwa viongozi wa Serikali, watendaji makundi maalum na viongozi wa kisiasa Mkoa wa Tanga.

Amesema kuwa katika matokeo hayo inaonyesha kuwa hali za uchumi wa wanawake zinakwenda kuimarika zaidi tofauti na hali ya sasa.

"Wanawake wanakwenda kushikilia uchumi kwani viashiria vinaonyesha kuwa hawachagui kazi za kufanya wanafanya kazi zote "amesema Kamisaa Makinda.

Hata hivyo Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga William Mwakilema amewataka wanawake kuyatumia matokeo ya sensa kujenga ajenda za kimkakati ikiwemo katika siasa, uimarishwaji wa huduma za kijamii sambamba na vita vya ukatili wa kijinsia.

"Zingatieni mafunzo hayo na kuongeza ufahamu wetu Ili tuweze kuwa uwelewa mmoja juu ya matokeo ya sensa katika utekelezaji wa majukumu yetu na utendaji ndani ya jumuiya zetu "amesema DC Mwakilema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live