Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Matibabu ya Himofilia kupatikana hospitali zote nchini

89d2fe7f413c89bf31824caa363a5179 Matibabu ya Himofilia kupatikana hospitali zote nchini

Tue, 13 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

HOSPITALI ya Taifa ya Muhimbili ipo mbioni kuanzisha kliniki kwa wagonjwa wa Himofilia katika hospitali zote za rufaa nchini kupitia mradi wa kuongeza kasi ya upatikanaji huduma kwa wagonjwa wa damu.

Himofilia ni ugonjwa wa damu kukosa uwezo wa kuganda ambao unasababishwa ukosefu wa kiwango cha kutosha cha chembechembe za protini zinazotakiwa kugandisha damu na kusababisha damu kuvuja kwa muda mrefu na upelekea mgonjwa kupoteza maisha.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Damu kutoka Muhimbili (MNH) Dk Stella Rwezaura amesema leo jijini Dar es Salaam katika mkutano uliwakutanisha madaktari wa hospitali zote za Dar es Salaam ambao wamebobea kwenye masuala ya damu.

“Lengo ni kuwafikia kwa urahisi wagonjwa wa magonjwa hayo ya damu ikiwemo himofilia na selimundu ili kuweza kupatiwa huduma kwa wakati, tofauti na ilivyo kwa sasa ambapo tiba hupatikana Muhimbili pekee.” alisema Rwezaura

Aprili 17 kila mwaka ni maadhimisho ya siku ya himofilia duniani ambapo utumika kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na ugonjwa huo.

Chanzo: www.habarileo.co.tz