Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Matatizo ya Mgongo, sekta ya mabenki yaongoza

56a78c569af1078bf4cd672b91c6015b Matatizo ya Mgongo, sekta ya mabenki yaongoza

Wed, 3 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

ASILIMI 80 ya wafanyakazi wa maofisini na viwanda wana matatizo ya mgongo na kusikia.

Hayo yamesemwa na Meneja wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), Jerome Materu katika mkutano wa wawekezaji ulioandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Godwin Gondwe kupitia kampeni ya 'One stop Jawabu' yenye lengo la Kusikiliza, Kutoa majawabu juu kero, changamoto inayomkabili wawekezaji wa Temeke.

Amesema sekta za mabenki zinachangamoto kubwa, na kwamba maofisi mengi viti vinavyowekwa na waajiri havizingatii masuala ya igonomia.

“Mabenki ndio wanaongoza kwa kuumwa migongo huku wafanyakazi wa viwanda wanaongoza kwa kutosikia kutokana na kelele za viwandani,”amesema Materu.

Amesema kikao cha wataalamu wa afya ambao wafanyakazi wanapelekwa na kampuni mbali mbali asilimia 80 ni watu wenye matatizo ya mgongo, na asilimia 20 wana matatizo ya kutokusikia sababu ya kelele sehemu za kazi.

“Wafanyakazi wa maofisini asilimia 80 wanapata matatizo ya mgongo kutokana na viti wanavyokalia ambavyo havizingatiii igonomia, na asilimia 20 ya wafanyakazi wanapata matatizo ya kusikia kutokana na kelele.” amesema Materu

Akifafanua Materu amesema katika maeneo ya kazi kuna viatarisha mbali mbali vya aina sita ambavyo ni viatarishi vya kemikali, kibaolojia, saikolojia, fizikia, na vya igonomia.

“Igonomia ni namna ya upangaji maeneo ya kazi, unawezaji kuwafahamisha wafanyakazi wako namna ya ubebaji wa mizigo iliyo salama, aina ya viti vinavyozingatia Igonomia ili asipate madhara.

“Lakini katika kuwahudumia wafanyakazi wengi tumegundua wana tatizo la mgongo kwa vile wanafanyakazi mahali ambako si salama, hapazingatii masuala ya igonomia, viti wanavyokalia ndio chachu kubwa ya matatizo, pia viwandani wananyanyua mizigo kwa kutumia migogo badala ya mikono.

Materu amesema tayari OSHA wameanza kutengenezea programu maalum kwa ajili ya kuwanusuru wafanyakazi mahali pa kazi kuepukana na changamoto kubwa inayowakabili ya kuumwa migongo.

“Tumeingia kwenye uchumi wa kati, rais anahimiza viwanda, sasa kama watanzania wana changamoto za kiafya hawawezi kufanya kazi, tunawaelimisha waajiri waweze kufuata muongozo wa mahali salama pa kazi.” amesema

Kwa upande wa Deogratius Lukomanyi akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya alisema kampeni ya ‘One Stop Jawabu’ ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya Rais John Magufuli kwa wateule wake ambapo amekuwa akiwahimiza kutokaa ofisini badala yake kuwafuata watu huko waliko na kuwahudumia pamoja na kutatua changamoto zao.

Amesema wameunganisha wafanyabiashara, wawekezaji, taasisi zote za umma, mashirika na taasisi binafsi ili zitatue changamoto zinazowakabili lengo ni kuweka mazingira mazuri ya kufanya biashara.

Chanzo: habarileo.co.tz