Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashine ya bilioni 15/- kuchunguza saratani

5768b2f6bfa0f200e563fbcda8a1f29a Mashine ya bilioni 15/- kuchunguza saratani

Mon, 23 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan amesema Serikali inatekeleza mradi wa kimkakati wa kufunga mashine ya kisasa ya upimaji magonjwa ya saratani katika hospitali ya Ocean Road Dar es Salaam itakayogharimu Sh bilioni 14.5. Samia pia alisema jana kuwa, Serikali imejipanga kuboresha huduma za afya zikiwemo za uchunguzi na matibabu ya saratani nchini ikiwemo ya shingo ya kizazi kwa lengo la kuongeza upimaji na uchunguzi mara mbili na kufikia wanawake milioni moja ifikapo 2025.

Akizungumza jijini Dodoma baada ya kushiriki mashindano ya mbio ndefu za NBC Dodoma Marathoni, Samia alisema mradi huo wa kimkakati unatekelezwa kwa fedha za ndani zilizotolewa serikali ili kupunguza mzigo wa gharama kubwa kupeleka wagonjwa wa saratani kutibiwa nje ya nchi.

“Serikali wa kimakakati wa kufunga mashine ya kisasa ya vipimo ya katika hsooitali ya Ovean Raad iliyogharimu sh bilioni 14.5 fedha zimetolewa na serikali ili kuhakikisha wagonjwa wa saratani wanapewa huduma nchini na kuipunguzia serikali mzigo mkubwa wa kupeleka wagonjwa nje ya nchi,” alisema. Pia alisema katika kupambana na maradhi hayo, uwekaji wa mashine za kisasa za tiba ya saratani katika hospitali ya Ocean Road umerahisisha upimaji wa magonjwa hayo kwa kiwango kikubwa.

Alisema serikali imejipanga kuboresha huduma za matibabu, huduma za uchunguzi na matibabu ya awali ili kupatikana kwa wananchi wote na lengo ni kuongeza idadi mara mbili ya wanawake wanaofanyiwa uchunguzi ili kufikia wanawake 1,000,000 ifikapo 2025.

Samia alisema serikali imeweka mkakati huo kwani hadi kufikia Juni 2020, vituo vya afya 649 vinatoa huduma za uchunguzi wa saratani ya uzazi ambapo katika mwaka 2019 wanawake 406,785 walifanyiwa uchunguzi ikilinganishwa na wanawake 127,188 waliofanyiwa mwaka 2015.

Aliwahakikishia Watanzania kwamba serikali itaendelea kuboresha huduma za upatikanaji wa huduma za uchunguzi, upimaji na matibabu ya saratani zinapatikana katika Hospitali za kanda ikiwemo ya Mwanza, (Bugando), Mbeya, Dodoma (Benjamin Mkapa), Kilimanjaro (KCMC) na Dar es Salaam (Ocean Road).

Samia alisema pia upatikanaji dawa za kutibu saratani ikiwemo ya shingo ya kizazi umeongezeka kutoka asilimia nne mwaka 2015 hadi 95 mwaka 2019.

Takwimu za hospitali ya Ocea Road zinaonesha kwamba asimilia 75 ya wanawake wanaofika katika hospitali hiyo wanafika wakiwa wamechelewa au ugonjwa upo katika hatua za juu ya tatu au ya nne hivyo kupunguza uwezekano wa kupona. Alisema saratani ni ugonjwa unaoathiri watu wote na rika zote na jinsia zote.

Kwani takwimu za Shirika la utafiti na Shirika la Afya Duniani (WHO) zilizotolewa mwaka 2018 zinaonesha kwamba kila mwaka hapa nchini kuna wagonjwa wapya 9,772 sawa wastani wa wagonjwa 59.1 katika kila watu 100,000. Alisema kati yao kila mwaka 6,695 kufariki dunia kutokana na saratani, tatizo hilo linazidi kuongezeka mwaka hadi mwaka.

Takwimu za mwaka 2019 zinaonesha kwamba wagonjwa wapya wa 13,215 walihudumiwa ambao ni sawa na 31 ya wagonjwa wapya waliohudumiwa katika mwaka 2019.

Alisema Tanzania inaongeza huduma za uchunguzi na upimaji ili kupatikana karibu na wananchi na inaendelea kushirikiana na sekta binafsi, mashirika ya kimataifa, yasiyo ya kiserikali na wadau wote kupambana na saratani.

Pia mpango wa kitaifa kwa kutoa chanzo za kukinga saratani mbalimbali ikiwemo na shingo ya kizazi unaendelea tangu umezinduliwa Aprili tangu 2018 ilipozinduliwa. Mpango huo unalenga kuwasaidia wasichana shuleni kuanzia miaka 14 na wa darasa la nne na tayari umewafikia zaidi ya asilimia 81.5 ya walengwa ili kusaidia kupunguza au kutokomeza ugonjwa wa shindo ya kizazi hapa nchini.

Samia alitoa mwito kwa wanawake kujitokeze kufanya uchunguzi wa mapema kujua afya zao na kama kuna tatizo hatua za matibabu zichukuliwe kwa haraka mapema.

“Nawaomba akina mama, akina mama wasiogope kwenda kufanya uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi,”alisema.

Samia aliipongeza benki ya NBC kwa kushirikiana na Shirikisho la Riadha Tanzania kuandaa mbio za aina hiyo kwa kusaidia kukusanya fedha zinazoshughulika na maradhi mbalimbali na kuimarisha kusongeza huduma za karibu na wananchi “Napongeza NBC kuchangia mapambano dhidi ya saratani kwa miaka mitano mfululizo ambapo asilimia 75 ya fedha husaidia kampeni ya saratani ya shingo ya kizazi.

Nimetarifiwa katika kipindi cha miaka miwili iliyobaki mnataka kuchangia kitu kingine ndani ya sekta ya afya,” alisema.

Makamu wa Rais aliwaomba wasibadili hata miaka miwili iliyobaki, waendelee kampeni hiyo ya mapambano dhidi ya shingo ya kizazi ambayo inasaidia aslimia 47 ya watu wanaoshambuliwa na maradhi hayo kwani. Pia alipongeza benki nyingine ikiwemo CRDB kwa kuwa Agosti mwaka huu ilikusanya fedha kusaidia taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.

Chanzo: habarileo.co.tz