Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Marumaru zatajwa kusababisha ugonjwa wa miguu, kisigino

50769 Pic+afya+marumaru

Sun, 7 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Marumaru imetajwa kuwa hatari kwa afya ya miguu na kisigino  kwani inasababisha ugonjwa wa miguu ambao kitaalamu unaitwa Calcunus Spur.

Hayo yamesemwa leo Jumamosi Apiril 6, 2019 na Ofisa Mfiziotherapia toka CCBRT Dk Focus

Magenge  wakati akizungumza na Mwananchi waliofika katika banda lao kupata huduma mbalimbali za afya katika kambi maalumu ya kupima afya iliyoandaliwa na Kampuni ya Mwananchi Comunications Limited (MCL) inayoendelea katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam,

Dk Magenge amesema watu wengi wamekuwa wakiabudu marumaru wanazoziweka ndani ya majumba yao kiasi cha kuvua viatu na kutembea peku muda wote bila kujua kuwa kufanya hivyo wanachuma maradhi ya miguu na kisigino.

"Marumarù zina athari kwa afya ya miguu kutokana na hali ya ugumu uliopo kwenye marumaru, mtu anapokanyaga unyayo wake moja kwa moja kwenye sakafu ya marumaru siku nzima  anapata msuguano wa misuli kamba ya unyayo hivyo kusababisha maumivu ambayo baadaye inaweza kusababisha mtu kushindwa kutembea," amesema.

Amesema ni bora mtu akatembea pekupeku kwenye vumbi kuliko kwenye marumaru  kwani marumaru haina sifa ya kubonyea hivyo humsababisha mtu kupata maumuvu.

Related Content

"Kuna tafiti nyingi zimefanyika juu ya marumaru na kuonekana zina madhara na hapa hospitalini tunapokea kesi nyingi za watu wenye matatizo ya miguu na unyayo ambayo yanasababishwa na marumaru.

Dk Magenge ameshauri ni  vyema mtu ambaye ameweka ma?umaru ndani ya nyumba  akavaa viatu muda wote ili kuzuia asipatwe na maradhi hayo," amesema.



Chanzo: mwananchi.co.tz