Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Marion Biontech yafungiwa India

Ert4 D Marion Biontech yafungiwa India

Mon, 27 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya India imeifuatia leseni Kampuni ya Marion Biontech baada ya dawa za Kikohozi zinazotengenezwa na Kampuni hiyo kuhusishwa na vifo vya idadi kubwa ya watoto kwenye nchi kadhaa vikiwemo vifo 18 nchini Uzbekistan.

Mwezi Januari mwaka huu Shirika la Afya duniani WHO, lilitoa tahadhari juu ya matumizi ya dawa za kikohozi zinazotengenezwa na Kampuni hiyo likizitaja kuwa chini ya viwango vinavyokubalika.

Baada ya vifo vya watoto hao, Wizara ya Afya ya nchini India iliamuru kusimamishwa kwa utengenezwaji wa dawa katika Kampuni hiyo.

Hata hivyo Jumatano hii mamlaka nchini humo imetangaza kuifuta kabisa leseni yao hivyo kuanzia sasa Kampuni hiyo hairuhusiwi kutengeneza dawa yoyote.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live