MAREKANI imeidhinisha chanjo ya ziada au ya Pfizer kwa watu wenye umri zaidi ya miaka 65, endapo walipata chanjo yao ya mwisho angalau miezi sita iliyopita.
Shirika la Marekani la Usimamizi wa Chakula na Dawa (FDA) pia limeidhinisha kwamba watu wazima walio katika hatari kubwa ya kuugua s na ambao wanafanya kazi zinazowafanya kuwa mstari wa mbele katika hatari kama wahudumu wa afya nao wapatiwe chanjo hiyo ya ziada.
Hatua hiyo, inamaanisha kuwa kwa sasa makumi ya mamilioni ya Wamarekani sasa wanahaki ya kupata chanjo yao ya tatu.
Hata hivyo, chanjo hizo bado zinahitaji idhini kutoka kwa Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC).
Majopo huru kutoka CDC yanafanya mikutano Jumatano na Alhamisi, na yanatarajiwa kuidhinisha hatua hiyo haraka, vyombo vya habari vya Marekani vinaripoti.
Uamuzi wa jopo utajumuisha mapendekezo juu ya nani anastahili kupata chanjo ya ziada kwa misingi ya kama aliye katika hatari zaidi, na ni wafanyakazi gani walio mstari wa mbele wanaostahili kupata chanjo hiyo kwanza.
Kwa upande wake, Kaimu Kamishna wa FDA Janet Woodcock alieleza kuwa wafanyakazi wanaotoa huduma za afya, walimu na wafanyakazi wanaotunza watoto, wafanyakazi wanaouza vyakula na wale walio katika vituo vya wasio na makazi au magereza wanapaswa kuwa kwenye orodha hiyo.
Hoja ya FDA ni ushindi kwa Rais wa Marekani Joe Biden, ambaye alikuwa ameahidi kuwa chanjo za ziada zitapatikana kuanzia mwezi huu pale tu itakapotolewa idhini kutoka kwa shirika la FDA na kituo cha CDC.