Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Marekani kuendeleza ushirikiano sekta ya afya

1dfb73b7b57859155996501666639bb9.jpeg Marekani kuendeleza ushirikiano sekta ya afya

Fri, 12 Nov 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Balozi wa Marekani nchini Donald Wright amesema nchi hiyo itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kukmarisha sekta za maendeleo ya jamii nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza (MPC) ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake mkoani humo alisema Marekani itaendelea kusaidia sekta ya afya ikiwamo kutokomeza magonjwa ya malaria.

Balozi huyo yuko mkoani hapa kukagua miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na Marekani.

Baadhi ya miradi ya maendeleo ambayo serikali ya Marekani imefadhili ujenzi wa maabara ya kisasa ya kupima vinasaba (DNA), ukimwi na Covid-19 katika hospitali ya Rufaa Bugando.

Mwenyekiti wa MPC Edwin Soko aliomba ubalozi huo kuendelea kusaidia nyanja ya habari katika kuwezesha kupata mafunzo yatakayoimarisha ubora wa sekta hiyo

Chanzo: www.habarileo.co.tz