Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manispaa ya Kinondoni yatakiwa kutengeneza chumba cha maiti

36741809b74623840e00772fcbd6ff1b Manispaa ya Kinondoni yatakiwa kutengeneza chumba cha maiti

Tue, 6 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Festo Ndugane ameitaka Manispaa ya Kinondoni kuweka mpango wa haraka kwa kutumia makusanyo ya ndani kujenga chumba cha kuhifadhia maiti katika Kituo cha Afya cha Kigogo.

Ndugane amebainisha hayo leo Jumanne bungeni jijini Dodoma alipokuwa anajibu swali la Mbunge wa Kinondoni, Abbas Tarimba (CCM) lililohoji ni lini Serikali itakipatia kituo hicho cha afya jokofu la kuhifadhi maiti ili kuwahifadhi watu waliotangulia mbele za haki.

“Naomba nitoe maelekezo kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Wilaya ya Kinondoni waweke mpango wa haraka waweze kujenga chumba cha kuhifadhia maiti katika kituo cha afya cha kigogo kwakuwa kituo hicho ni muhimu na kinawahudumia wakazi wa wilaya tatu ambazo ni Kinondoni, Ilala na Ubungo” amesema Ndugane.

Aidha, Ndugane amesema kuwa wilaya hiyo ina mwenendo mzuri katika ukusanyaji wa mapato hivyo anaamini ujenzi huo hautawashindwa.

Chanzo: www.habarileo.co.tz