Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mamilioni ya punda wachinjwa kutengeneza dawa

Pundapic Mamilioni ya punda yachinjwa kutengeneza dawa

Fri, 16 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Steve ambaye ni mkazi wa jiji la Nairobi nchini Kenya alitegemea biashara ya kuuza maji ili kupata mkate wake wa kila siku.

Alikuwa akitumia punda kukokota mkokoteni uliokuwa na uwezo wa kubeba madumu 20 ili kusambaza maji kwa wateja wake.

Lakini kuna hii siku ambayo mkazi huyo aliamka na kukuta punda wake wote wakiwa wameibwa.

"Sikuwaona punda wangu," anasema. "Niliwatafuta siku nzima, usiku kucha na siku iliyofuata. Nilichanganyikiwa."

Siku tatu baadaye anasema alipigiwa simu na rafiki yake akimwambia ameona mifupa ya wanyama anaoamini ni punda wake.

"Walichinjwa, wakaacha minofu na mifupa. Hakukuwa na ngozi."

Wizi wa punda kama aliokutana nao Steve umeongezeka katika siku za karibuni sehemu nyingi za Afrika na kwingineko duniani.

Asili ya uhitaji mkubwa wa punda hadi watu kuwa tayari kuwaiba haianzii Kenya bali China.

Hii ni baada ya kuwepo kwa dawa ya jadi inayoitwa Ejiao yenye asili ya China inayotengenezwa kutokana na ngozi ya punda.

Inaaminika kuwa na dawa hiyo inaimarisha afya na kumfanya mtu aonekana kijana. Pigia msitari maneno ‘aonekane kijana’.

Ngozi za punda huchemshwa na kisha hutengenezwa poda, vidonge au dawa ya majimaji na wakati mwingine hutumika kwa kuongezwa kwenye chakula.

Katika ripoti mpya, wanaharakati wamekuwa wakifanya kampeni dhidi ya biashara hiyo ya punda tangu 2017.

Inakadiria kuwa duniani kote takribani punda milioni 5.9 huchinjwa kila mwaka ili kupata dawa hiyo.

Inadaiwa kwamba matumizi ya dawa hiyo yamekuwa yakiongezeka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live