Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mamia wajitokeza kupima afya bure jijini Mwanza

73561 Mwanza+pic

Fri, 30 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Mamia ya wakazi wa Jiji la Mwanza nchini Tanzania wamejitokeza kupima afya bure katika  Hospitali binafsi ya Uhuru ya jijini humo.

Huduma hiyo ya siku mbili kuanzia leo Ijumaa Agosti 30, 2019 itakayohusisha upimaji wa maradhi mbalimbali inatolewa katika kituo kipya cha hospitali hiyo kilichopo eneo la Iseni kata ya Butimba jijini Mwanza.

Makundi ya wananchi wanaohitaji huduma yalianza kujikusanya eneo hilo tangu saa 12:00 asubuhi huku wafanyakazi wa hospitali hiyo wakiendelea na maandalizi ya huduma.

Mwenyekiti wa kamati ya huduma, Dk Jaonithe Mlaki amesema huduma hiyo yenye kauli mbiu ya “Mtu ni afya summit” inalenga kuwasaidia watu wenye kipato cha chini kupata vipimo vya maradhi ambavyo baadhi ni ghali na hawawezi kuzimudu gharama zake.

“Huduma itatolewa na Wataalam Bingwa wa maradhi mbalimbali wakiwemo wale wa magonjwa ya moyo, masikio, koo, mifupa, macho, meno, afya ya uzazi,” amesema Dk Mlaki

Amesema pamoja na mambo mengine, huduma hiyo itakayotolewa kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni ni kurejesha sehemu ya faida kwa jamii kama shukrani.

Pia Soma

Advertisement   ?

Mmoja wa wananchi walijitokeza kupata vipimo, Hosea Maliganya ameziomba hospitali nyingine, zikiwemo zile za rufaa za mikoa na kikanda kutenga siku maalum kwa ajili ya huduma za bure za vipimo kwa wananchi wa kipato cha chini wasiomuda gharama kubwa za vipimo.

“Ni rahisi kutima maradhi pale yanapogundulika mapema kuliko kusubiri hadi mtu aanze kuumwa; tunaomba huduma za namna hii ziwe endelevu kwa hospitali zote binafsi na za umma,” amesema Maliganya

 

Chanzo: mwananchi.co.tz