Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mamia wajitokeza kupima afya bure Mtwara

76543 Pic+mamia

Fri, 20 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mtwara. Mamia ya wakazi wa Mtwara nchini Tanzania wamejitokeza katika kituo cha afya cha Likombe mkoani humo kwa ajili ya kupima magonjwa mbalimbali na kupatiwa tiba.

Hatua hiyo imekuja baada ya Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani kwa kushirikiana na kampuni ya usafirishaji ya Machinga na kituo cha Ilala Afya Centre kuweka kambi ya siku mbili kwa ajili ya huduma mbalimbali kwa wakazi wa mkoa wa Mtwara kwa kushirikiana na madaktari toka Dar es Salaam.

Huduma zinazotolewa ni pamoja na upimaji wa shinikizo la damu, tezi dume, kisukari, saratani ya matiti na saratani ya mlango wa kizazi.

Huduma nyingine zitakazotolewa ni macho na miwani na meno kwa makundi mbalimbali.

Mmoja wa wanufaika wa huduma ya upimaji wa macho, Amina Mileka amesema huduma hiyo ni nzuri na kuomba muda uongezwe.

“Huduma ni nzuri lakini siku mbili hazitoshi kwa sababu watu ni wengi na wengine wa vijijini bado hawana taarifa hivyo wakisikia watakuwa wengi,” amesema Mileka

Pia Soma

Advertisement
 

Mmoja wa madaktari wanaotoa huduma kutoka Ilala Afya Centre, Dk Tariq Azizi amesema hadi kufikia saa nne tayari wameshawaona wagonjwa zaidi ya 1,000 na kwamba kutokana na wingi wa watu wanakusudia kuwahudumia hadi watu 1,500.

“Tulianza shughuli saa moja lakini hadi kufikia saa 4:30 asubuhi tumeshaona wagonjwa zaidi ya 1,000 nahisi kwa leo tunaweza kuwaona wagonjwa 1,500 hadi 2,000 kutokana na idadi ya watu kuwa kubwa,” amesema Dkt Aziz

Amesema katika idadi ya watu waliojitokeza wengi ni wa matatizo ya shinikizo la damu, kisukari na macho.

“Tunashukuru serikali kwa kutupatia wafanyakazi na eneo nzuri kwa ajili ya kutoa huduma, changamoto kubwa tuliyokutana nayo ni utoaji wa dawa kwa sababu ya wingi wa watu.”

“Tumeshindwa kuwapa dozi ya muda mrefu na kuwapa ya mwezi mmoja mmoja lakini tunaowakuta na matatizo tunawapendekezea kwenda kwenye vituo vya jirani ili kuendelea kupata tiba endelevu,” amesema Dk Aziz

Chanzo: mwananchi.co.tz