Dar es Salaam. Mamia ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wamejitokeza katika Hospitali ya Aga Kkhan kufanyiwa uchunguzi wa homa ya ini.
Leo Jumamosi Julai 27, 2019 Mwananchi limeshuhudia wakazi hao, wengi wakiwa wanawake wakijitokeza kwa wingi katika upimaji huo ikiwa ni siku moja kabla ya maadhimisho ya kimataifa ya kupambana na ugonjwa huo.
Akizungumza na Mwananchi leo daktari bingwa wa mfumo wa chakula na ini wa hospitali hiyo, Casmir Wambura amesema mwitikio wa watu umekuwa mkubwa mno.
Amebainisha kuwa walipanga kufanya uchunguzi huo kwa watu wasiozidi 400 lakini hadi kufika saa nne asubuhi zaidi ya watu 800 wamejitokeza.
“Ni jambo ambalo limetupa imani kwamba elimu kuhusu ugonjwa huu imefika na watu wameanza kuelewa hatari yake kiasi cha kuwahi kuchunguza afya zao,” amesema Wambura.
Amesema asilimia 80 ya watu wenye ugonjwa huo duniani hawajitambui kwa kuwa hawajafanya uchunguzi wa afya wala kupata chanjo.
Pia Soma
- Ujumbe wa Mbatia kwa Rais Magufuli huu hapa
- Magufuli kuelekeza nguvu Tazara, atoa maagizo wizara ya fedha
- Mkuu wa wilaya ya Chemba afungua kesi, ataka kuwataliki wake zake wawili
- Trump atoa kauli kesi ya rapa Asap
Faida Haji, mkazi wa Kimara ni miongoni mwa waliojitokeza kuchunguza afya na kueleza kuwa awali hakufahamu athari za ugonjwa huo.