Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mambo ya kawaida yanayoboresha afya

13931 Dk+CHRIS TanzaniaWeb

Mon, 27 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mara nyingi tumekuwa tukidharau mambo madogo madogo ambayo yapo ndani ya uwezo wetu kuyatekeleza ambayo kupitia hayo, tungeweza kuzinufaisha afya zetu kwa kiasi kikubwa sana na kujiepusha na magonjwa hasa yasiyo ya kuambukiza.

Wengi wetu tumejikuta tukipata maradhi mbali mbali na kulazimika kubeba mzigo mkubwa wa matibabu lakini huenda kinga yake ni kufuata tu masharti madogo madogo sana ya kiafya ambayo kwa udogo wake hayalingani na ukubwa wa matibabu unaolazimika kujitwika baada ya homa.

kufanya maamuzi sahihi ya aina ya chakula ili kuepukana na madhara ya kiafya yatokanayo na ulaji wa vyakula ambavyo si salama.

Jumuika na wengine

Jenga tabia ya kuondokana na upweke mara kwa mara na ujumuike na watu wanaokuzunguka. Kwa kufanya hivi utajiweka kwenye nafasi nzuri ya kuepukana na matatizo ya kisaikolojia kama vile sonona (depression) na hata msongo wa mawazo.

Lakini kwa kufanya hivi itakusaidia kuyamudu matatizo mengine ya kiafya kama vile shinikizo la damu na magonjwa mengine ya kiakili. Sio lazima uwe na watu wengi sana wa kujumuika nao, hata wachache tu ambao upo karibu nao wanaweza kuleta mabadiliko makubwa kwako zaidi ya ujuavyo.

Kujumuika na watu hata kwa masaa machache kunaongeza furaha, na kisayansi pia imethibitika kunaongeza utendaji kazi wa vichocheo vinavyoleta hisia mwilini na hivyo kukufanya uwe na hari ya kufanya jambo husika. Hivyo ita marafiki na ujumuike nao kwenye chakula cha jioni na hata sehemu yeyote ya kupumzisha akili angalau mara moja kwa wiki.

Kabili msongo wa mawazo na kila kitu kinachoingilia furaha yako

Moja ya vitu muhimu tunavyowahimiza sana watu ni kujitahidi kuishi maisha yenye afya bora. Lakini ukweli ni kwamba hamna maisha yenye afya bora pasipokuwa na furaha.

Ieleweke kuwa, kukosa furaha kunaweza kusababisha matatizo mengi na makubwa sana kiafya zaidi ya vile unavyoweza kufikiria. Hata sisi wahudumu wa afya huwa tunakutana na changamoto kubwa sana kuwatibu wagonjwa wenye matatizo ya kisaikolojia na hasa waliokosa furaha kuliko wagonjwa wa aina nyingine yeyote ile.

Kila mmoja amewahi kupitia hali hii. Lakini msongo wa mawazo ukizidi unaweza kusababisha kukaza kwa mishipa ya damu na kuongezeka kwa kasi ya mapigo ya moyo, ambayo yakidumu sasa hupelekea matatizo kama vile magonjwa ya moyo na hata shinikizo la damu.

Hivyo ni vyema kuyatambua mambo yanayokatisha furaha yako mara kwa mara na uweze kukabiliana nayo.

Kujipa muda wa kutosha wa kulala

Nadhani msomaji unafahamu faida za kiafya za kupata usingizi kwa muda wa kutosha. Lakini kuna faida nyingine nyingi sana za kiafya zilizopo kwenye jambo hili.

upata muda wa kutosha wa kulala haina maana kwamba ulale usiku na mchana, hapana! Bali ujipe masaa mengi ya kulala wakati usiku. Kiafya inashauriwa binadamu anatakiwa kupata muda usiopungua wa masaa manane ya kulala kwa usiku mmoja. Tabia ya kujinyima muda wa kutosha wa kulala kwa muda mrefu inaweza kusababisha matatizo kadha wa kadha ya kiafya kama vile shinikizo la damu, kisukari na hata baadhi ya matatizo yanaoenda kuathiri afya ya akili yakiwemo sonona (depression), na matatizo ya kusahau.

Bila shaka hukulijua hili. Hivyo jenga tabia ya kupata muda wa kutosha wa kulala ili uweze kuepukana na matatizo haya na kupata faida nyingine nyingi za kiafya ambazo hukuwahi kuzifikiria.

Chanzo: mwananchi.co.tz