Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maji yanayohitajika ili figo zako ziendelee kuwa imara

Maji Ya Kunywa.jpeg Maji yanayohitajika ili figo zako ziendelee kuwa imara

Mon, 8 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Unakunywa maji kiasi gani kwa siku? Kama ulikuwa hujui wataalamu wa afya wanashauri ili figo zako ziendelee kuwa imara unapaswa kunywa maji lita moja kwa kila kilo 25 za mwili wako.

Hii ina maanisha kuwa kama uzito wako ni kilo 50 utapaswa kunywa maji lita 2 kwa siku na iwapo kilo zako ni 75 lita tatu zinakufaa kwa saa 24.

Kwa mujibu wa wataalamu, unywaji mwingi wa maji huzuia mawe kwenye figo, husafisha madini ya sodiamu na urea na inashauriwa kunywa kiasi hicho ili kufikia kiasi cha mkojo cha angalau lita 2.0 hadi 2.5 kwa siku ili kuzuia maradhi katika figo.

Hayo yamesemwa leo Jumatatu, Januari 8, 2024 na Mtaalamu wa afya ya jamii, Dk Ali Mzige alipokuwa akielezea changamoto za kuongezeka kwa wagonjwa wa figo nchini na magonjwa yasiyoambukiza.

Amesema iwapo mtu ana uzito wa kilogramu 62 anapaswa kunywa maji lita 2.53 ambayo ni sawasawa na vikombe vya chai sita mpaka vinane.

“Kwa kunywa hivyo unajaribu kuokoa figo zako, unajaribu kuweka mwili wako katika hali nzuri na unajaribu kuimarisha afya yako kwa sababu asilimia 60 ya uzito wako ni maji, kwahiyo kila kitu mwilini kina namna yake ya kujiendesha,” amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live