Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majeraha ya uti wa mgongo na mambo ya kuzingatia

5b81288b9dc252bb5b08b3e17d78ac6a Majeraha ya uti wa mgongo na mambo ya kuzingatia

Thu, 10 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

AJALI za barabarani zinatajwa kuwa chanzo kikubwa cha ongezeko la watu wanaosumbuliwa na majeraha kwenye uti wa mgongo duniani yanayowasababishia ulemavu.

Ingawa sababu za ajali hizi zinaweza kuwa ni ubovu wa barabara, lakini asilimia kubwa husababishwa na uzembe wa madereva na upuuzwaji wa sheria za usalama barabarani.

Jeraha katika uti wa mgongo ni uharibifu wa aina yoyote unaotokea kwenye uti wa mgongo kwa sababu yoyote ile na kuleta madhara katika mfumo wa utendaji wa viungo vya mwili wa mtu.

Mara nyingi hali hii husababisha mtu kubadilika kabisa kwa mfumo wa maisha yake kutokana na kushindwa kutembea. Ripoti ya Shirika la Afya Duniani inaonesha kusababisha kiharusi.

Anasema maeneo mengine ya mwili pia yanapata matatizo kama ini, figo na mapafu na kwamba wenye ugonjwa wa Ukimwi au kisukari huathirika zaidi na kwamba ni rahisi pia mgonjwa kupooza.

Mbali na maumivu makali na kupungukiwa damu, Dk Malangahe anasema wakati mwingine macho ya watoto hugeuka kuwa njano. Dk Malangahe anasema ili kuwa na uhakika ni vizuri kwenda hospitalini kupima vipimo vinavyogharimu Sh 40,000 ili kuepuka mtoto anayepata ugonjwa huo kulazwa mara tatu kwa mwaka hospitalini kutokana na kupungukiwa damu.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tiba kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee, Dk Sara Maongezi wakati anafungua mafunzo kwa waandishi kuhusu magonjwa yasiyoambukiza anasema, mwezi Septemba kila mwaka ni wa Maadhimisho ya Sikoseli Duniani.

Anasema Tanzania inaadhimisha kwa kutoa elimu kwa umma kuhusu ugonjwa huo na kuhamasisha jamii kupima kama ina vinasaba vya sikoseli ili kutibu mapema kabla hata ya kuoana.

Dk Maongezi anasema, ugonjwa huo wa kurithi unawakumba zaidi watoto wa chini ya miaka mitano, hasa katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo ambayo ndio wakati ambao seli huwa zinabadilika ili kuundwa kwa seli za utu uzima.

Mratibu wa Sikoseli Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Asteria Mpoto anasema wizara inafanya jitihada kubwa kuhakikisha dawa ya kutibu ugonjwa wa sikoseli ya hydro-urea inapatikana kwa urahisi madukani.

Anasema dawa hiyo, kwa sasa inauzwa Sh 2,000 kila kidonge na mgonjwa anahitaji vidonge vitatu kwa siku hivyo anatakiwa awe na Sh 6,000 kila siku na kuitumia maisha yake yote.

Anasema kuiingiza dawa hiyo kwenye mfumo wa dawa ambazo mtu anaweza kutibiwa kwa kutumia bima ya afya itakuwa msaada mkubwa kwa wanaotumia bima hiyo.

“Tumeshawaandikia Bohari ya Dawa kuhakikisha dawa hizi zinapatikana kwa wingi katika maeneo mbalimbali nchini,” anasema.

Anamaliza kwa kusema kwamba wananchi wanapoona dalili za watoto kuwa na macho ya njano, kulalamika maumivu au kupungukiwa damu ni vema kwenda kupima afya zao ili kujua kama wana sikoseli kwani ni ugonjwa ambao unatibika.

Majeraha ya uti wa mgongo na mambo ya kuzingatia kwamba kati ya watu 250,000 na 500,000 duniani hupatwa na majeraha kwenye uti wa mgongo kila mwaka kutokana na sababu mbalimbali.

Huku ajali, hasa za barabarani zikiongoza, sababu nyingine za majeraha kwenye uti wa mgongo zinazotajwa ni magonjwa na vitendo vya ukatili.

Ripoti hiyo pia inaonesha kwamba vijana wa kiume wa umri wa kati ya miaka 20 hadi 29 ndiyo wako katika hatari kubwa hasa katika nchi za Afrika na Asia kutokana na mtindo wa maisha ulivyo ambapo asilimia kubwa hutumia vyombo vya moto hasa pikipiki.

Uchunguzi wangu unaonesha kwamba hata idadi kubwa ya vijana wenye umri huo jijini Dar es Salaam ni watumiaji wa usafiri wa pikipiki, hali inayowaweka pia katika hatari ya kupata ajali.

Tatizo lililopo ni kwamba waendesha bodaboda wengi hawazingatii kanuni za usalama barabarani na baadhi yao huendesha huku wakiwa wametumia vilevi mbalimbali.

Dk Leonard Makey, mtaalamu wa tiba kwa njia ya mazoezi katika hospitali ya KCMC mkoani Kilimanjaro, anasema kama ilivyo kwa maeneo mengine, wamekuwa pia wakipokea wagonjwa wenye matatizo ya uti wa mgongo.

Anasema asilimia kubwa ya wagonjwa wanaopokea huwa wametokana na ajali za bodaboda ikifuatiwa na ajali za kuanguka kwenye miti, hususani wakati wakivuna maparachichi.

Rais wa Chama cha Kimataifa cha wenye majeraha ya uti wa mgongo (International Spinal Cord Injury Society), Dk H. S. Chhabra, anasema jeraha la uti wa mgongo ni kitu hatari sana kwa mustakabali wa maisha ya mtu kwani huharibu kabisa mfumo wa utendaji wa mwili wake.

“Utendaji wa viungo vya mwili unakuwa umeharibiwa na kusababisha kushindwa kufanya kazi kwa ufasaha. Mtu akishapatwa na hali hiyo ni vigumu kuikubali kwa haraka.

Inamchukua muda kuzoea na kuanza kupambana na changamoto mbalimbali atakazoendelea kukutana nazo,” anasema Dk Chhabra. Anaongeza: “Ukipata jeraha kwenye uti wa mgongo unashindwa kufanya kazi na hivyo kuendeleza kuingiza kipato kama ulivyozoea lakini pia unapambana na gharama za matibabu ambazo ni za juu pia.”

Ripoti za kitabibu zinaonesha kuwa mtu anaweza kuepuka kupata madhara makubwa ya jeraha la uti wa mgongo ikiwa atawahi kufanyiwa upasuaji ndani ya saa 72 baada ya kupata ajali na kugundua amepata jeraha katika eneo hilo muhimu sana la mwili.

Mtu anaweza kupata madhara makubwa zaidi ikiwa atakosa matibabu sahihi kwa wakati sahihi na hivyo kuwahishwa hospitali ya uhakika kwa mtu aliyepata ajali bila kujali amepata majeraha kiasi gani ni jambo la muhimu sana ili kupunguza hatari za mtu kupata ulemavu.

Mariam Kassimu ni mmoja wa waathirika na shuhuda wa tatizo la jeraha la uti wa mgongo ambaye amekuwa akiishi kwa msaada wa kiti cha magurudumu kwa muda wa miaka tisa sasa.

Ni kiti hicho kinachomsaidia kutoka eneo moja kwenda jingine. Mariam ambaye ni mkurugenzi wa taasisi inayoshughulika na waathirika wa majeraha ya uti wa mgongo nchini inayotambulika kwa jina la Mariam Spinal Cord Injury Foundation anaeleza changamoto alizokutana nazo tangu alipopata tatizo hilo hadi kuamua kuanzisha taasisi hiyo.

“Nilizaliwa nikiwa mzima na viungo kamili na nimeishi maisha yangu yote nikiwa mzima. Nilikuwa mwanafunzi wa chuo tena nikiwa na najishughulisha na biashara, nilikuwa ni msichana mwenye ndoto kama wengine mpaka ilipofika Desemba 4, 2011 mambo yalipobadilika baada ya kupata ajali ya gari.

“Ajali ilinisababishia majeraha lakini kubwa nilijeruhiwa uti wa mgongo na kujikuta naishia kwenye kiti cha magurudumu baada ya kufanyiwa upasuaji na kuwekwa vyuma vinane mgongoni.

Haikuwa rahisi kukubali kwamba nilikuwa nimepoteza uwezo wa kutembea kabisa. Ni hali ambayo ilikuwa inanikatisha tamaa kabisa lakini kwa ushirikiano wa watu wa ustawi wa jamii pale Muhimbili na daktari wangu, Nicephorus Rutasibwa nikaanza kubadili mtazamo.

“Ilinichukua miaka miwili kukubali kabisa kwamba hakuna namna nyingine bali ni kuishi na hali hii katika mtazamo chanya. Wakati huo nikiwa nimeshapambana sana na changamoto nyingi.

Baadhi hizo ni kumpoteza mwanaume niliyekuwa naye na kushindwa kusimamia biashara nilizokuwa ninafanya.

“Kwa kuwa nilikuwa nimeambiwa nizingatie mazoezi uwezekano wa kupona upo, hivyo nikaelekeza akili na nguvu zangu zote katika kufanya mazoezi na hivyo nikaamua kuuza biashara zangu kwa dada yangu ili nipate muda wa kufanya mazoezi,” anasema.

Mariam anasema akiwa wodini wakati anauguzwa alianza kuona baadhi ya wagonjwa wakiwa wanakosa mahitaji muhimu yakiwemo maji na hivyo akawa analazimika kuwaomba ndugu zake wagawe vitu walivyokuwa wanamletea kwa wagonjwa wengine.

Anasema baada ya kutoka hospitali na kukubaliana na hali halisi alianza kufikiria namna alivyokuwa akiwashuhudia wale watu waliokuwa wanakosa mahitaji na wengine wakiwa wamepoteza matumaini na hapo ndipo wazo la kuanzisha taasisi ya Mariam lilipomjia.

“Nakumbuka nilianza na wazo la kutoa kile kiti cha magurudumu ambacho nilitoka nacho hospitali kwa sababu kuna mgonjwa mmoja ambaye alikuwa hana kiti cha magurudumu, nikaamua kumpa lakini niliporudi hakuwepo nikampatia mwingine niliyemkuta.

“Baadaye nikasajili Foundation ya Mariam, nikaanza kufanya kazi ya kuwahudumia waathirika wa jeraha la uti wa mgongo kwa kuwatembelea majumbani na hospitalini kuwatia moyo, kuwapa utayari wa kuishi na hiyo hali lakini pia kuangalia changamoto zao za kiuchumi na kuona namna ya kuzitatua.

“Tumekuwa tukiangalia namna ya kuwabadilisha, yaani kuangalia ni kitu gani kingine mtu anaweza kufanya akiwa na hali ya ulemavu ukiachana na shughuli walizokuwa wanafanya awali kisha tunawawezesha kwa kuwapa mitaji,” anasema.

Mariam anaiomba Serikali iangalie namna itakavyoweza kusogeza huduma za upasuaji wa uti wa mgongo karibu zaidi na wanachi ili kuwawezesha kupata matibabu ya upasuaji ndani ya saa 72 zinazopaswa kwa sababu wengine hupatwa na ulemavu kwa sababu ya kuchelewa kupata matibabu.

Halikadhalika, anaziomba asasi zisizo za kiserikali na wamiliki wa viwanda vya vifaa tiba kuona namna wanavyoweza kuzalisha vyuma vinavyotumika katika matibabu ya jeraha la mgongo ili kupunguza gharama za sasa ambapo vyuma hivyo vinatoka nje ya nchi.

Anawahimiza pia wananchi wote kuwapenda na kuwapa msaada watu waliopata majeraha kwenye uti wa mgongo na kuwasaidia kadri wanavyoweza ikiwemo matibabu na viti vya magurudumu hadi mitaji ili waendelee na maisha kama watu wengine.

Chanzo: habarileo.co.tz