Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahitaji ya Chanjo ya COVID-19 vituoni yazidi idadi ya watu

D0b7592f9cd4fb36c3180a42ac1bc1e7 Wananchi wajitokeza kupata Chanjo

Wed, 4 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamia wamejitokeza kupata chanjo katika mikoa mbali mbali ya Tanzania Akizungumza na Mwananchi jana, Ofisa elimu wa afya kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk Tumaini Haonga alisema tangu chanjo hiyo izunduliwe na kutangazwa vituo vya kutolea kumekuwa na mwitikio mkubwa wa watu wanaohitaji.

Alisema katika mfumo wa Tehama ambao unapokea maombi kuna idadi kubwa ya maombi, huku kwenye vituo vya afya navyo kuna waliokwenda kujiandikisha ili kupatiwa chanjo hiyo inayoanza leo kutolewa katika mikoa mbalimbali nchini. a vituo 28 vya kutoa chanjo hiyo mkaoni humo.

Wakati huohuo chanjo dhidi ya virusi vya corona ukianza leo nchini kote, chanjo hizo zimeanza kugombewa, baada ya makundi ya watu kujitokeza kujiandikisha kuzipata.

Tanzania ilipokea awamu ya kwanza ya msaada wa dozi 1,058,400 za chanjo za corona aina ya Johnson & Johnson iliyotolewa na Marekani kupitia mpango wa Covax Facility.

Rais Samia Suluhu Hassan alizindua chanjo hiyo Julai 28, jijini Dar es Salaam kwa kuchanjwa, akifuatiwa na viongozi na watendaji wa Serikali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live