Ulaji wa maharage meupe kwa wingi watajwa kuwa msaada katika kuondoa na kupunguza uwezekano wa kupata maambukizi ya saratani ya utumbo.
Utafiti uliofanywa na madaktari wa Kituo cha Saratani cha Chuo Kikuu cha Texas umegundua kujumuisha maharage hayo aina ya ‘ Navy Beans au Haricot Beans’ kwa walioathirika na saratani utumbo huboresha kinga mwili na kuzuia kujirudia kwa saratani hiyo.
‘Colorectal cancer’ ni saratani ambayo huathiri utumbo mpana na ni saratani inayoshika nafasi ya tatu kati ya saratani zinazofahamika zaidi duniani. Saratani hii hutibika kabisa katika hatua za awali lakini pia, ina tabia ya kurudi tena ndani ya miaka mitatu baada ya operesheni ya kwanza na ulaji wa maharage meupe husaidia zaidi kuepusha kujirudia kwa saratani hii kwa kiwango kikubwa ukilinganisha na ulaji wa maharage mengine.
Katika kupambana na saratani ya utumbo mazoezi na lishe bora hutajwa, ingawa madaktari hao wa Texas wanashauri msisitizo zaidi kuwekwa akwa wagonjwa kuongeza ulaji wa maharage.