Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magufuli atoa Sh4bilioni ujenzi hospitali ya Mkoa Simiyu

16328 Simiyu+pic TanzaniaWeb

Sun, 9 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Simiyu. Rais John Magufuli amesema atatoa Sh4bilioni kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya Hospitali ya Mkoa wa Simiyu.

Ametoa ahadi hiyo leo Jumamosi Septemba 8, 2018 katika uzinduzi wa jengo la wagonjwa wa nje la Mkoa huo mjini Bariadi.

Amesema ataipatia hospitali hiyo kiasi hicho cha fedha ili zisaidie ujenzi wa majengo haraka kwa kuwa wananchi wanapata shida kupata huduma za afya.

“Mwanzo  walikuwa hawataki nifungue, kwa sababu mimi najua nikawaeleza nitafungua hata kama bado haijakamilika ndio maana nimekuja,” amesema.

Amesema kutokana na umuhimu shirika la Global Fund limechangia Sh1.1bilioni kwa ajili ya sekta ya afya.

Awali, akitoa taarifa ya jengo la wagonjwa wa nje la Mkoa wa Simiyu, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema limegharimu Sh3.1bilioni.

Amesema ujenzi huo ulianza 2015 na kwamba unatarajiwa kumalizika 2019.

Ummy amesema katika bajeti ya mwaka 2018/19, Serikali imetenga Sh1.5bilioni kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo.

Amesema kwa sasa wameshaanza kutoa huduma za upimaji, ushauri nasaha na kutoa dawa kwa wagonjwa.

Chanzo: mwananchi.co.tz