Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magufuli achangia Sh400 milioni za ujenzi kituo cha afya, atoa maagizo kwa mawaziri

68257 Jpm+pic

Thu, 25 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, John Magufuli ameahidi kutoa Sh400 milioni kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya cha Kisaki kilichopo mkoani Morogoro huku akiwataka wakazi eneo hilo kuchapa kazi.

Magufuli ametoa ahadi leo Alhamisi Julai 25, 2019 wakati akizungumza na wananchi eneo la Kisaki lililopo katika halmashauri ya Morogoro vijijini huku akitoa agizo kwa mawaziri wake, Ummy Mwalimu (afya) na Seleman Jafo wa Tamisemi kuhakikisha wanasimamia ujenzi huo haraka.

Kiongozi huyo mkuu wa nchi alikuwa safarini kwenda Rufiji kwa ajili ya kwenda jiwe na msingi la mradi wa kufufua umeme wa megawati 2115 wa Strigle’s Gorge uliopo mikoa ya Pwani na Morogoro.

Mkuu huyo wa nchi amefikia uamuzi huo, baada ya wakazi hao kumweleza hawana kituo cha afya katika eneo hilo.

“Kwanini  hakuna kituo cha afya na kuna watu wengi hapa? Nataka kituo cha afya kianze kujengwe mara moja nitamuagiza Waziri wa  Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi) ashughulikie.”

“Nawapa siku saba tafuteni eneo, tujenge hospitali ambayo imejengwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk John Magufuli,” amesema Magufuli huku akishangaliwa na umati wa wakazi wa Kisaki waliojitokeza kumsikiliza.

Pia Soma

Pamoja na kutoa mamilioni hayo, Magufuli ameendesha harambee ya  kuchangia ujenzi wa kituo cha polisi ambapo ameanza kwa kuchangia Sh5 milioni.

Katika harambee hiyo, Sh34 milioni zimechangwa ikiwamo ahadi ambapo ametoa amesema keshokutwa Jumamosi ya Julai 27, 2019 ujenzi uwe umeanza na ndani ya siku saba waliotoa ahadi wote wawe wamekamilisha ahadi zao.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz