Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magonjwa ya ngono yaongezeka

Ummy Mwalimu Jk Magonjwa ya ngono yaongezeka

Fri, 12 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Idadi ya watu waliougua magonjwa ya ngono imeongezeka kutoka wagonjwa 458,61 katika kipindi cha kati ya Januari mwaka 2021/22 hadi 480,448 katika kipindi kama hicho mwaka 2022/23.

Hayo yamesemwa leo Ijumaa Mei 12, 2023 na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu wakati akisoma makadirio ya mapato na matumizi ya mwaka 2023/24.

“Magonjwa ya ngono yaliyoongoza ni Klamidia (Chlamydia), Kaswende (Syphilis) Kisonono (Gonorrhea) na Herpes,”amesema Ummy.

Aidha, Ummy amesema ili kuwakinga watoto wachanga kuzaliwa na maambukizi ya magonjwa ya ngono ambapo wajawazito milioni 1.09 sawa na asilimia 65 walipimwa maambukizi ya Kaswende ikilinganishwa na wajawazito milioni moja sawa na asilimia 66 katika mwaka 2021/2022.

Amesema wajawazito 11,068 sawa na asilimia moja ya wajawazito wote waliopimwa walibainika kuwa na maambukizi ya kaswende na walianzishiwa tiba ikilinganishwa na wajawazito 10,535 sawa na asilimia moja kwa kipindi kama hicho mwaka 2021/2022.

“Nitumie fursa hii mbele ya Bunge lako Tukufu kuwaelewa wananchi kuwa magonjwa ya ngono bado yapo hivyo wanapaswa kuchukua hatua za kujikinga na endapo watapata maambukizi kuwahi kwenda kwenye vituo vya kutoa huduma ili wapate tiba sahihi na mapema,”amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live