Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magonjwa ya moyo, kisukari yasumbua wengi

Ee5044e4364ab2c7e741f3fb34cbd86e.jpeg Magonjwa ya moyo, kisukari yasumbua wengi

Fri, 12 Nov 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Magonjwa wa moyo na kisukari ni miongoni mwa magonjwa yasiyoambukiza yanayoongoza kuwa

na wagonjwa wengi kutokana na mfumo wa maisha wa sasa.

Mtaalamu kutoka Chama cha Kisukari (TDA), Dk Rachel Nungu alisema akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Arusha katika wiki ya magonjwa yasiyoambukiza.

Alisisitiza umuhimu wa kula vyakula halisi katika makundi matano ikiwemo kuacha matumizi ya tumbaku, pombe na dawa za kulevya.

Alisema katika maad- himisho hayo ya magonjwa yasiyoambukiza, kwa kushirikiana na Shirikisho la Vyama vya Magonjwa yasiyoambukiza (TANCDA), wanapima watu mbalimbali kisukari, shinikizo la damu na visababishi vya magonjwa yasiyoambukiza.

“Ugonjwa wa moyo, kisukari na shinikizo la damu ndio magonjwa yanayoongoza, hivyo nashauri watu wafanye mazoezi na kuzingatia mlo kamili na kue- puka tabia bwete,” alisema.

Alisema kwa mujibu wa utafiti wa mwaka 2012, kila watu 100 wenye miaka 25 na kuendelea, watu tisa wana kisukari, 26 wana shinikizo la damu, watu 25 mafuta yaliyozidi kwenye damu na 34 wana uzito uliozidi.

Alisisitiza watu kupenda kutembea kwa miguu badala ya kuendesha magari. Alishauri pia wanapokuwa ofisini wasimame au kutembea mara kwa mara ikiwemo kupata nafasi ya kula matunda au vyakula vyenye lishe bora.

Chanzo: www.habarileo.co.tz