Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magonjwa ya mlipuko kudhibitiwa

Gonjwa Pic Data Magonjwa ya mlipuko kudhibitiwa

Thu, 17 Feb 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Vifaa hivyo vitakavyogawiwa kwenye mikoa 18 nchini vimetolewa leo Februari 17, 2022 na Shirika lisilo la kiserikali la "Management and Development for Health –(MDH)" kupitia ufadhili wa rasilimali fedha na ushauri wa kitaalamu kutoka kituo cha kudhibiti magonjwa cha Marekani-CDC, ofisi ya Tanzania.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Mkurugenzi wa Oparesheni wa MDH Dk Nzovu Ulenga amesema hatua hiyo imekuja baada ya kuona uwepo wa magonjwa ya mlipuko yaliyojitokeza hivi karibuni ambayo yanahitaji vifaa madhubuti kwa ajili ya kudhibiti na kukusanya takwimu kwa haraka.

“Ufuatiliaji huu utasaidia kukusanya data mapema, kuzihifadhi na kuzisambaza ili kusaidia kupunguza kasi ya maambukizi kwa wananchi wengine kuchukua hatua mapema hususan kwa magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya hewa”amesema

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi msaidizi Epidemiolojia na udhibiti wa magonjwa kutoka Wizara ya Afya, Dk Rogath Kishimba baada ya kupokea vifaa hivyo amesema vitakwenda kusaidia kukusanya na kutoa taarifa rasmi za magonjwa yanayoambukiza.

“Natoa Shukran kwa shirika la kudhibiti na kuzuia Magonjwa pamoja na shirika la MDH kwa kutoa vifaa hivi vitakavyo kwenda kurahisisha utendaji kazi na kuwahudumia wagonjwa kwa haraka” amesema Dk Kishimba

Advertisement Vifaa hivyo vilivyotolewa vitasaidia katika kupambana na magonjwa ya mlipuko, katika maeneo matatu ambayo ni uwezo wa kutambua  visababishi vya magonjwa, kutoa taarifa kwa haraka na kuchukua hatua sahihi za kupambana na ugonjwa husika kwa kufuata taratibu za nchi na za kimataifa.

Vifaa vilivyotolewa kwenye makabidhiano hayo ni pamoja na Kompyuta mpakato (laptops), vishwikwambi (tablets), projekta, Mashine ya kuchapa (Printers) na vifaa mbalimbali vya steshenari kwa ajili ya kazi za machapisho ya ripoti za kisayansi na maabara

Chanzo: www.mwananchi.co.tz