Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maghala makubwa ya kuhifadhia bidhaa za afya kujengwa Dodoma

Maghala Makubwa Ya Kisasa Ya Kuhifadhia Bidhaa Za Afya Kujengwa Dodoma.jpeg Maghala makubwa ya kuhifadhia bidhaa za afya kujengwa Dodoma

Fri, 11 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bohari ya Dawa (MSD) imeingia mkataba na kampuni ya Hainnan International kwa ajili ya ujenzi wa maghala ya kisasa (WiB)kwa ajili ya uhifadhi wa bidhaaa za afya, Kanda ya MSD Dodoma.

Akizungumza wakati wa utiaji saini wa mradi huo, Meneja Miradi wa MSD, Deo Orauya ameeleza maghala hayo yatakua kitovu (hub) cha uhifadhi na usambazaji wa bidhaa za afya kwenye Kanda nyingine za MSD hasa zinazohudumia Kanda ya Kati, Kanda ya Magaharibi, na Nyanda za Juu Kusini.

Amefafanua kutokana na ongezeko la watu na ujenzi vituo vipya vya kutolea huduma za afya nchini, MSD imejidhatiti kuongeza uwezo wake wa uhifadhi, ili kuendana na mabadiliko hayo kwa kujenga maghala ya kisasa, ambapo pia utasaidia uhifadhi na usambazaji wa bidhaa za afya nchini.

Pamoja na hayo amesema makabidhiano ya eneo la ujenzi, yameongozwa na mshauri mwelekezi Architect Nkini kutoka kampuni ya ABECC, inayomilikiwa na Chuo Kikuu cha Ardhi -Dar es Salaam.

Ujenzi wa maghala hayo yenye ukubwa wa sqm elfu 5, katika kiwanja na.92/1&2/Kizota Dodoma, jirani na Ofisi za Kanda za MSD, unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 10, huku ikiakisiwa huenda ujenzi ukakamilika ndani ya muda mfupi zaidi ya huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live