Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magari ya wagonjwa 195 kupelekwa Halmashauri 184

Ambulance 195 Magari ya wagonjwa 195 kupelekwa Halmashauri 184

Thu, 23 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imesema itanunua magari 195 ya kubebea wagonjwa ambayo yatapelekwa kwenye halmashauri 184 nchini kote zikiwemo Halmashauri za wilaya ya Liwale Nachingwea na Kilwa.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa TAMISEMI DKT. Festo Dugange wakati akijibu swali la Mbunge Tecla Mohamed aliyetaka kufahamu mpango wa serikali katika kuzipatia magari ya wagonjwa hospitali za wilaya ya Liwale, Nachingwea na Kilwa.

Naibu Waziri Dugange amesema katika mwaka wa fedha 2021/22 kupitia mpango wa maendeleo kwa ustawi wa taifa na mapambano dhidi ya uviko 19 itanunua magari hayo 195.

Aidha Dkt. Dugande amesema katika mgao wa magari hayo kuna halmashauri zitapata gari zaidi ya moja kutokana na idadi ya watu waliopo katika eneo pamoja na umbali wa utoaji huduma katika hospitali.

Sambamba na hayo serikali imesema itanunua magari mengine 204 kwa ajili ya shughuli za usimamizi wa sekta ya afya pamoja na kurahjisisha utoaji wa chanjo kwa watoto.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live