Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maeneo hatari kwa dengue Dar

56895 Pic+dengue

Mon, 13 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Serikali imeyataja maeneo yaliyoathirika zaidi na homa ya dengue jijini Dar es Salaam na imeweka bayana kuwa vipimo vya ugonjwa huo kwa sasa vinatolewa bure kwa mgonjwa atakayethibitisha kwamba amepewa rufaa kutoka kituo cha kutolea huduma ngazi ya chini.

Kwa mujibu wa takwimu kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, jumla ya watu 1,200 wameugua homa hiyo jijini humo, huku mmoja akipoteza maisha. Hii ni kwa kipindi cha Januari hadi Mei mwaka huu.

Akizungumza na Mwananchi jana, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dk Yudas Ndugile alisema kadri muda unavyozidi kwenda wagonjwa wengi zaidi wanagundulika ikilinganishwa na hali ilivyokuwa Januari na Februari.

Maeneo hatari

Dk Ndugile alitaja maeneo na kata zilizopata wagonjwa wengi zaidi kuwa ni Ilala, Kariakoo, Upanga, kisutu, Buguruni, Tabata, Mbezi, Ubungo, Kinondoni, Msasani na Masaki.

“Maeneo haya tajwa yamegundulika kuwa na wagonjwa wengi zaidi hivyo hatua zinapaswa kuchukuliwa ili kudhibiti maeneo hayo ikiwamo wananchi wenyewe kuchukua hatua,” alisema.

Pia Soma

Jinsi ya kuepuka

Kwa mujibu wa wataalamu, homa ya dengue inaweza kuepukwa kwa kuzuia kuumwa na mbu anayesambaza virusi vinavyo sababisha ugonjwa huo.

Dalili za dengue

Mtu anaweza kutambua kuwa ameambukizwa kwa kuhisi dalili kama homa kali ya ghafla, maumivu makali ya kichwa, macho kuuma, maumivu ya viungo, kichefuchefu, kutapika, vipele ambavyo hutokea siku nne baada ya homa kuanza. Ugonjwa ukiwa mbaya zaidi, mtu anaweza kutokwa damu puani, kwenye fizi na kuchubuka kirahisi.

Mwa mujibu wa Dk Ndugile, tayari vitendanishi nimeelekezwa katika hospitali maalum na wanaohisiwa kuugua watafikishwa huko kwa rufaa.

“Vipimo ni bure, lakini kwa kuwa dalili za homa ya Dengue zinafanana sana na za magonjwa mengine kama malaria, wataalam wa afya katika kituo hivyo watafanya uchunguzi zaidi kabla ya kufikia hatua ya kumpima homa hiyo,” alisema.

Hospitali hizo ni na Amana, Temeke, Mwananyamala, Mnazi Mmoja, Bombo na hospitali ya mkoa wa Singida.

NHIF yatoa vipimo bure

Wagonjwa ambao ni wanachama wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wanaweza kutibiwa homa ya dengue bila kutoa pesa mfukoni wanapofika kituoni. Awali, kulikuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wagonjwa waliofika katika vituo vya huduma kutozwa fedha hata kama ni wanachama wa mifuko ya bima ya afya hasa ile ya binafsi.

Taarifa iliyotolewa jana na kitengo cha mawasiliano NHIF imeeleza kuwa, mfuko huo kwa kushirikiana na hospitali za umma katika mikoa iliyoainishwa unaandaa utaratibu kwa wanachama wake kupata huduma ya kipimo cha homa ya dengue bure katika mikoa iliyoathirika.

Jinsi ya kudhibiti Dengue

Dk Ndugile alisema wananchi wanapaswa kuangamiza mazalia ya mbu kama vifuu, makopo, vyungu chakavu, matairi chakavu, kufukia madibwi na kufyeka nyasi kwenye maeneo ya makazi, ofisini, shule, vyuo, garage, stendi za mabasi, masoko, mama ntilie, baa, pub, hoteli, migahawa na hosteli.

“Wanachi wanapaswa kuzuia kung’atwa na mbu kwa kutumia chandarua kitandani, kupaka mafuta ya kufukuza mbu mikononi na miguuni, kuvaa nguo ndefu kufunika mwili kama mikono, miguu na mgongo,” alisema.

Chanzo: mwananchi.co.tz