Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maelfu wanufaika mpango wa CHF

7e20ddd4eb2cec9ee470141d5ff6820e Maelfu wanufaika mpango wa CHF

Tue, 22 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kaya 50,600 mkoani Morogoro zimeandikishwa na kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Aidha, mfuko huo umefanikiwa kulipa Sh milioni 197.5 ambayo ni malipo ya ruzuku kwa vituo vya kutolea huduma za afya kuanzia Januari hadi Juni 2021.

Akitoa taarifa kwenye mkutano wa nusu mwaka wa tathmini ya utekelezaji wa mfuko na mkataba wa lishe, Mratibu wa Mfuko huo Mkoa wa Morogoro, Elisia Mtesigwa alisema kaya hizo zilizoandikishwa ni sawa na asilimia 10 ya zote 590,065 zilizopo mkoani hapa.

Aliwashauri viongozi wa ngazi mbalimbali mkoani huo kuendelea kuhamasisha wananchi wajiunge na mfuko huo kwani una gharama ndogo ya matibabu.

Alisema mkoani Morogoro, mchango wa kujiunga ni Sh 30,000 na mwanachama atanufaika na matibabu kwa watu sita kwa mwaka mzima na mahala popote nchini.

Alishauri halmashauri za wilaya kuimarisha asilimia ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba. Pia alisisitiza asilimia ya dawa muhimu iongezwe hadi kufikia asilimia 100.

Kuhusu malipo ya Sh milioni 197.5 kwa vituo vya huduma za afya, alisema zaidi ya kiwango kilichotolewa Julai hadi Desemba 2020/2021 ambayo yalikuwa Sh milioni 167.3 kwa vituo vya kutolea huduma za afya mkoani humo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live