Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maduka ya dawa yasiokidhi vigezo yafungwa

Duka La Dawazz.jpeg Maduka ya dawa yasiokidhi vigezo yafungwa

Sun, 20 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Mwantum Mgonja ametoa maagizo kwa Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo na Wataalamu wake kuchukua hatua mara moja ya kuyafunga maduka yote ya dawa yaliyokaguliwa na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) na kukosa vigezo huku akiwataka wamiliki wote kufuata sheria za Nchi.

Mwantum Mgonja ameyasema hayo wakati wa kikao cha Kamati ya Chakula na Dawa (CFDC) ya Halmashauri hiyo ya Mkuranga na Wawakilishi wa TMDA.

Katika kikao hicho alipokea ripoti ya ukaguzi uliofanywa na TMDA kwenye maduka ya dawa za binadamu na mifugo, ukaguzi uliofanyika Machi 14-18 mwaka huu na kukuta mapungufu mbalimbali ikiwemo kukutwa na dawa zilizokwisha muda wake, huku mengine kutokuwa na watoa dawa waliopata mafunzo.

"Nakuagiza Mganga Mkuu kuhakikisha ndani ya Halmashauri hii ya Mkuranga, maduka yote ambayo hayana vibali na hayataki kufuata taratibu yafungiwe haraka sana kuanzia sasa napotoa taarifa hii lakini kingine nimezuia maduka ya dawa ambayo yanauza yakiwa hayana Wataalamu, tunawaita 'Famasia', Mtu anafungua duka lake la dawa lakini anaenda kuuza dawa kienyeji, yale maisha ni maisha hatarishi, tunahatarisha wananchi wa Wilaya hii ya Mkuranga lakini pia tunahatarisha maisha yetu sisi binafsi ambao ni wakazi wa hapa Mkuranga"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live