Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madiwani walalamikia wajawazito kutozwa fedha

9f247f5afad01163451598c719abc65f Madiwani walalamikia wajawazito kutozwa fedha

Fri, 12 Aug 2022 Chanzo: Habari Leo

Madiwani wa Halmshauri ya Wilaya ya Bariadi, mkoani Simiyu, wamelalamikia kitendo kinachofanywa na baadhi ya wahudumu wa afya kuwatoza fedha wajawazito wakati wa kujifungua katika vituo vya afya na zahanati za serikali wilayani Bariadi mkoani Simiyu.

Pia wamelalamikia hali ya kukosekana kwa baadhi ya vifaa tiba na dawa, ambavyo hutumiwa na wajawazito, wakati au mara baada ya kujifungua.

Sophia Nhandi Diwani Viti Maalumu Kata ya Gideshi, anasema alienda kujifungua katika hospital Kata ya Dutwa na kukuta wajawazito wanatozwa fedha.

"Wajawazito wakienda kujifungua wanatozwa fedha, mfano Zahanati Kata ya Dutwa kuna baadhi ya kinamama walitozwa fedha Sh 10, 000 hadi Sh 20,000, ili apatiwe huduma na kujifungua," alisema.

Kwa upande wake, Diwani Viti Maalumu Kata ya Dutwa, Mwamba Sayi, alisema wamebaini baadhi ya wanawake wanatozwa gharama za vifaa kama Mpira wa kujifungulia na baadhi yao wamekuwa wakiombwa Sh 10,000 hadi Sh 20,000, ili wapatiwe huduma hiyo.

Naye Duka Mashauri Mapya, Diwani wa Kata ya Mwagabhana, Alisema kuwa anasikitishwa na hali ya vituo vyao vya kutolea huduma ni duni, hasa katika suala la dawa, wengi wamekuwa wakiandikiwa kwenda kununua dawa maduka binafsi.

Akijibu hoja za Madiwani hao, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Bariadi Dk. Ipilila Zambi, alisema mjamzito anapoenda kujifungua hatozwi fedha na huduma zote ni bure.

Lakini anasema wanapopenda kliniki huwa wanataarifiwa baadhi ya vitu vichache wanavyotakiwa kujiandaa navyo.

"Huduma za kujifungua hizi ni bure na hakuna fedha yoyote anayotozwa kwa ajili ya kupata huduma hiyo, japo huwa tunawashauri kujiandaa kwa baadhi ya vifaa kama delivery bag, ambayo mzazi hutakiwa kuwa nayo," alisema.

Chanzo: Habari Leo