Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madiba wamshukuru JPM kuboresha sekta ya afya

43e37469b812e19d66a1adb402d548fb Madiba wamshukuru JPM kuboresha sekta ya afya

Mon, 30 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

HALMASHAURI ya Madaba katika Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma, imemshukuru Rais John Magufuli kwa mchango mkubwa aliotoa wa kuboresha na kuimarisha sekta ya afya katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Shafi Mpenda, wakati akiongea na Habarileo ofisini kwake katika Mji Mdogo wa Madaba wilayani Songea.

Mpenda alisema katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Rais Magufuli alitoa jumla ya Sh milioni 900 ambazo zimefanikisha kujenga Kituo cha Afya Mtyangimbole kwa kujenga majengo mapya kwa gharama ya Sh milioni 500 na Kituo cha Afya Madaba kwa kuongeza majengo sita kwa Sh milioni 400 ambayo yameboresha utoaji huduma kwa wananchi.

Alisema kujengwa kwa vituo hivyo vya afya kumeimarisha na kuchochea watumishi wa afya kufanya kazi kwa bidi pamoja na kuongeza ari ya wananchi kwenda kupata huduma za matibabu katika vituo hivyo tofauti na hapo awali.

Mpenda alisema halmashauri yake ina watumishi wa afya wa kutosha wakiwemo madaktari kwa kuwahudumia wananchi zaidi ya 2,335 kutoka jimbo la Madaba.

“Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais Magufuli kwa upendo wake mkubwa kwa wananchi wa Madaba, ametupatia Sh milioni 900 ambazo zimesaidia kuboresha sekta ya afya katika halmashauri yetu,”alisema Mpenda.

Sambamba na Sekta ya Afya, alisema Serikali ya Awamu ya Tano pia imefanya kazi kubwa ya kuboresha Sekta ya Elimu kwa kutoa fedha za kutosha zilizotumika kujenga vyumba vya madarasa, mabweni na nyumba za walimu katika maeneo mbalimbali.

Chanzo: habarileo.co.tz