Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madhara 5 ya kutafuna kucha na jinsi ya kuacha

Nails Madhara 5 ya kutafuna kucha na jinsi ya kuacha

Tue, 30 Aug 2022 Chanzo: Swahilitimes

Watoto wengi na vijana wamekuwa wakipitia hali hii ya kutafuna kucha, lakini wengi wao kadri wanavyokua huiacha tabia hii.

Wataalamu wanasema hakuna sababu ya moja kwa moja ambayo hupelekea mtu kutafuna kucha, ila kuna sababu ambazo huweza kuchangia tabia hii kama msongo wa mawazo, kukosa utulivu na wasiwasi pamoja na kuhusishwa na matatizo ya afya ya akili.

Haya ni baadhi ya madhara yatokanayo na utafunaji wa kucha:

Unapokula kucha unaweza kuwa kwenye hatari ya kupata fangasi (fungal infections) hasa kwenye ‘nail plate.’

Kupata magonjwa kutokana na vimelea kama vile bakteria pamoja na virusi kutoka kwenye kucha kwenda mdomoni.

Unaweza kusababisha madhara kwenye meno kama vile; meno kuchimba, mpangilio mbaya na kuathiri fizi.

Kusababisha michubuko mdomoni, kwenye fizi za meno n.k.

Kumeza kucha zilizong’atwa zinaweza kuongeza hatari ya maambukizi tumboni.

Njia za kujizuia kutafuna kucha

Kama unatamani wewe au mwanao kuacha kula kucha, unaweza kufuata hatua zifuatazo:

Kaa mbele ya kioo na kisha jiangalie unapokuwa unakula/kutafuna kucha uone jinsi unavyoonekana.

Kata kucha ili ziwe fupi, na kisha zisawazishe vizurii ili kusiwe na ncha mbazo zitakushawishi kuzitafuna.

Kwa wasichana, pendelea kupaka rangi kucha zako ili kuzuia kutamani kuzitafuna.

Jaribu kuipatia kazi mikono, chezea kalamu au nunua mpira mdogo ili kukifinya unapohisi hamu ya kula kucha.

Tafuta ”gum” ambazo hazina sukari utafune badala ya kutafuna kucha.

Endapo tatizo hili litazidi unashauriwa kumuona daktari kwaajili ya vipimo ikiwemo vipimo vya afya ya akili.

Chanzo: Swahilitimes