Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madaktari wapangua hoja chanjo ya corona

13eb0e7aa8719f2cc64e413d1c5b346d Madaktari wapangua hoja chanjo ya corona

Fri, 30 Jul 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WATAALAMU wa afya wamesema kitendo cha watu kutoiamini chanjo dhidi ya virusi vya corona kwa kigezo cha muda uliotumika kuitengeneza si jambo la msingi.

Mkurugenzi wa Kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Leonard Subi alisema jana Dar es Salaam kuwa chanjo inaweza kutengenezwa ndani ya mwaka mmoja na inatengenezwa kuzingatia mfumo sahihi wa kisayansi.

“Sayansi haina siasa, maprofesa wanashinda maabara, mpaka sasa chanjo bilioni sita zimeshachanjwa duniani.” alisema Dk Subi na kuongeza;

“Kuna mafua ya ndege ni makali kama ilivyo corona, tafiti zinaendelea, kwenye janga la mlipuko wanasayansi wanaunganisha nguvu, mpaka sasa chanjo 280 zimeshazalishwa ila zilizopitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO), ni chanjo nane tu,”

Dk Subi alihimiza wananchi waende kupata chanjo ya corona ili hata wakiambukizwa virusi yasiwe maambukiz makali kiasi cha kushindwa kufanya kaz.

Profesa Karim Manji kutoka Idara ya Magonjwa ya Watoto, Chuo Kikuu cha Sayansi Shirikishi (MUHAS) alisema Dar es Salaam kuwa Covid si ugonjwa mpya na teknolojia imekua hivyo mijadala kwamba umetumika muda mfupi kupata chanjo kukabili Covid-19 haina mashiko.

Alisema kama viashiria vipo, vinyemelezi vipo, teknolojia ipo chanjo inaweza kutengenezwa kwa miezi sita hadi mwaka mmoja.

“Chanjo inaweza kutengenezwa ndani ya muda mfupi, mambo yamebadilika na sayansi imezidi kubadilika hususani kwa magonjwa yanayoua haraka kama ebola, corona na mengineyo,”alisema Profesa Manji na kuongeza;

“Enzi za nyuma mtu alikuwa akitaka kupasha chai inabidi awashe moto, lakini sasa hivi unaweka kwenye microwave, sayansi inabadilika kutoka kuchukua muda mrefu hadi muda mfupi hasa katika majanga ya dharura. Siku za nyuma insulin ilitokana na homoni ambayo inatengenezwa kwenye kongosho la binadamu, ili kudhibiti sukari, lakini sasa hivi insulin inatengenezwa maabara,”

Chanzo: www.habarileo.co.tz