Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madaktari wa KCMC kuhudumia albino bure

11178 Kcmc+pic.png TanzaniaWeb

Tue, 10 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tanga. Madaktari bingwa wa Hospitali ya Rufaa KCMC mkoani Kilimanjaro wanatarajia kutoa huduma na uchunguzi wa saratani ya ngozi kwa watu wenye ualbino mkoani Tanga.

Nuru Kilima, anayeratibu huduma hiyo alisema jana kuwa itatolewa kuanzia leo katika wilaya za Tanga, Muheza, Korogwe, Lushoto na Handeni.

Kilima ambaye ni mwenyekiti wa chama cha watu wenye ualbino wilayani Korogwe, alisema huduma zitakazotolewa bure ni tiba ya ngozi kwa walioathiriwa na mionzi ya jua, watapatiwa mafuta maalumu kwa ajili ya kuzuia mionzi hiyo.

Naye mkazi wa Makorola jijini Tanga, Daud Juma mwenye ualbino alisema huduma hiyo inatolewa wakati sahihi kwa sababu wengi wao hawana uwezo wa kumudu gharama za matibabu na hata kununua vifaa vya kujikinga na mionzi ya jua.

Chanzo: mwananchi.co.tz