Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madaktari bingwa figo, moyo kupelekwa hospitali za mikoa

304a6f40c968ae3de93beb52c276b570 Madaktari bingwa figo, moyo kupelekwa hospitali za mikoa

Tue, 8 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameomba wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro kukipa ridhaa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kiunde serikali ili ikamilishe mchakato wa kupeleka madaktari bingwa wa magonjwa moyo, fi go, mifupa na saratani katika hospitali za mikoa. Majaliwa aliyasema hayo kwenye mkutano wa kumuombea kura mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, John Magufuli, mgombea ubunge Moshi Mjini, Priscus Tarimo na wagombea udiwani.

Mkutano huo ulifanyika kwenye Viwanja vya CCM Kata ya Majengo mjini Moshi. Alisema mpango huo una lengo la kuwapunguzia wananchi gharama za kwenda Dar es Salaam na nje ya nchi kufuata tiba. “Serikali ya Awamu ya Tano imefanya makubwa na wote ni mashahidi na mojawapo ni imefanikiwa kutibu magonjwa ya moyo, figo na saratani katika Hospitali ya Taifa Muhimbili...miaka ya nyuma Watanzania walitumia mamilioni ya fedha kutafuta matibabu nje ya nchi,” alisema.

Alisema serikali inatarajia kupeleka madaktari bingwa kila mkoa ili kuboresha zaidi sekta ya afya, ambayo imekuwa na changamoto kwa Watanzania kumudu gharama. “Pamoja na kuwepo kwa vifurushi vipya vya bima ya afya (NHIF) bado serikali inatafiti huduma bora zaidi zinazotolewa na mfuko huo ambazo zitahusisha Watanzania wote ili kuwarahisishia kupata matibabu bora zaidi kuliko hali ilivyo sasa,” alisema.

Alisema Serikali ya Awamu ya Tano ina mambo mengi ya kujivunia katika sekta za elimu, miundombinu, miradi kikubwa ya maji, umeme, viwanda na madini, ambayo haijawahi kufanyika kwa muda mrefu.

Majaliwa aliomba wananchi wamchague mgombea ubunge wa Moshi Mjini, Tarimo ili akamilishe mchakato wa manispaa hiyo kuwa jiji. “Manispaa ya Moshi ina sifa zote za kuwa jiji, hospitali, miundombinu ya barabara, idadi ya wakazi na huduma nyingine muhimu... ili muwe jiji jibu lake analo Tarimo, CCM tunaomba, mtumeni mgombea huyu akamilishe kazi,” alisema.

Chanzo: habarileo.co.tz