Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madaktari bingwa Italia kushiriki vita magonjwa yasiyoambukiza

10222 Madaktari+%255Dpic TZW

Fri, 29 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wakati tafiti zikionyesha kuwa ifikapo mwaka 2020 asilimia 73 ya vifo vyote duniani vitatokana na magonjwa yasiyoambukizwa, Taasisi ya madaktari bingwa wa Italia wanaohudumia Afrika (CUAMM) wamesema wapo tayari kuisaidia Tanzania kupambana na magonjwa hayo.

Akizungumza juzi katika hafla iliyofanyika bustani ya nyumbani kwa Balozi wa Italia, Oysterbay jijini hapa, meneja mkazi wa taasisi hiyo, Matteo Capuzzo alisema wataipa ushirikiano Tanzania endapo itahitaji.

“Kwa kweli sasa kasi ya ongezeko la magonjwa yasiyo ya kuambukizwa ni kubwa duniani kote ikiwamo hapaTanzania na kwa asilimia kubwa yanatokana na mtindo wa maisha yetu watu, tupo tayari kusaidia kinga hata na kutibu lakini jambo la msingi ni kuelimisha watu kuhusu magonjwa hayo,” alisema Capuzzo.

Alifafanua kuwa watasaidia kwa kuwaleta madaktari wao bingwa ili kutibu na kubadilisha ujuzi na wataalamu wa afya wazawa lakini pia kuelimisha watu kuhusu namna ambavyo wanaweza kujikinga na magonjwa hayo.

“Kikubwa wananchi wanapaswa kufuata matakwa ya kiafya, kubadili mtindo wa maisha, kufanya mazoezi na kula vizuri,” alisema Capuzzo.

Naibu mkurugenzi wa huduma za kinga kutoka Wizara ya Afya Dk Leonard Subi alisema kuna vifo vingi vitokanavyo na magonjwa hayo lakini mapambano yake yanahitaji ushiriki wa watu wote.

“Watu wengi hawafanyi mazoezi lakini pia mpangilio wa chakula si mzuri ndiyo maana magonjwa hayo yanazidi kushamiri hivyo nitoe rai kwa kila Mtanzania kujali afya yake,” alisema Dk Subi.

Chanzo: mwananchi.co.tz