JUMLA ya madaktari Bingwa 11 wa Mifupa na Ubongo kutoka Jamuhuri ya Watu wa China wamewasili katika Taasisi ya tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) ambapo watakuwa wakitoa huduma kwa miaka miwili.
Hatua hiyo ya kupokelewa na madaktari hao ni muendelezo wa ushirikiano baina ya Tanzania na China.
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa hafla fupi yakuwapokea madaktari hao kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, Mkurugenzi wa Upasuaji wa Ubongo MOI, Dk Lemeri Mchome ameishukuru serikali ya Jamhuri ya Watu wa China na kuongeza kuwa ujio huo utaongeza ujuzi na umahiri kwa madaktari wazawa.
“Wenzetu China wamepiga hatua katika tiba za mifupa, ubongo na mishipa ya fahamu, hivyo uwepo wao hapa utasaidia kuwajengea uwezo kwa madaktari wetu, ninaaamini walivyotukuta sivyo ndivyo watakavyotuacha, umahiri wetu utakuwa umepanda” amesema Dk Mchome.