Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madaktari Mloganzila wapatiwa mafunzo ya upasuaji

Mlonganzilaa Madaktari Mloganzila wapatiwa mafunzo ya upasuaji

Thu, 2 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Madaktari Bingwa wa Upasuaji Hospitali ya Taifa Muhimbili (Upanga & Mloganzila) wamepatiwa mafunzo kwa vitendo kuhusu namna ya kufanya upasuaji mdogo (Procedure) inayoitwa AVF (Arterial Venous Fistula Creation) na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Mishipa ya damu na Upandikizaji wa Viungo Prof. Park Kwan Tae kutoka Korea kusini kwa ufadhili wa Shirika la KOFIH.

Upasuaji huo ambao wanafanyiwa wenye changamoto ya Figo ambao wapo kwenye matibabu ya kuchuja damu (Dialysis), unasaidia kuunganisha mshipa unaotoa damu kwenye Moyo na kusambaza kwenye mwili (Ateri) na Mshipa unaorudisha damu kwenye moyo (Vein) hivyo kusaidia wagonjwa hao kutokuwekewa Cetral Catheter ambayo inachangamoto nyingi wakati wa utunzaji wake ambapo inaweza kupelekea mgonjwa kupata maambukizi ya bakteria.

Mafunzo hayo ya siku tano yanahusisha Madaktari Bingwa wa Upasuaji Upanga na Mloganzila ambapo yatafanyika kwa muda wa miezi miwili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live