Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madaktari Bingwa wa moyo wapiga kambi Tabora

Madaktari Bingwa Wapiga Kambi, Waanza Upasuaji Tabora.png Madaktari Bingwa wa moyo wapiga kambi Tabora

Thu, 18 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya wataalamu wakiwemo wadaktari bingwa wa magonjwa ya Moyo kutoka katika Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo jijini Dar es salaam wanaendelea na matibabu ya kibingwa ya magonjwa hayo katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete.

Matibabu hayo ambayo yamekusanya mamia ya wakazi wa mkoa wa Tabora na mikoa jirani ya Singida ,Kigoma na Shinyanga yanaendelea katika hospitali hiyo kwa muda wa siku tano ambapo yatamalizika Januari 19 ,2024

Wakizungumzia namna ambavyo zoezi hilo linavyo endelea mmoja wa madaktari bingwa wa magonjwa ya ndani ya moyo Mlangwa Lucas amesema matibabu hayo maarufu kama Dkt. Samia Suluhu Hassani tiba mkoba yamelenga kuwasaidia wananchi ambapo katika kipindi cha siku tatu wamewafikia wagonjwa watu wazima zaidi ya 80 huku baadhi yao wakipewa maelekezo ya kwenda rufaa kwa ajili ya matibabu zaidi katika taasisi hiyo.

Akieleza kuhusu tatizo la moyo kwa watoto Daktari bingwa Parvina Kazahura amesema katika kipindi cha siku tatu wamewafikia watoto zaidi ya 28 ambapo watoto 9 wamegundulika wakiwa na shida ya moyo .

Hata hivyo amesema matatizo ya moyo kwa watoto kabla ya kuzaliwa yamekuwa yakitokana na akinamama wajawazito kuvuta sigara ,kunywa vilevi na vihatarishi vingine ikiwemo mionzi .

Kwa upande wake afisa lishe wa taasisi hiyo ya moyo Husna Yasin amesema magonjwa ya moyo kwa watu wazima ,zaidi yamekuwa yakisababishwa na tabia za maisha ya kila siku ikiwemo kutokuzingatia ulaji wa unaokubalika kiafya .

Chanzo: www.tanzaniaweb.live