Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madaktari 24 kutoka Korea watua Dar, kutoa huduma Buchosa

Batch 20220702 153359 768x576 Madaktari 24 kutoka Korea watua Dar, kutoa huduma Buchosa

Sat, 2 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jopp la madaktari 24 kutoka Korea Kaskazini, leo Julai 2, 2022 wamewasili nchini na kupokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, ambapo wataelekea katika Jimbo la Buchosa, Sengerema jijini Mwanza ambapo watatoa huduma mbalimbali za kitabibu kwa wakazi wa maeneo hayo.

Akizungumza wakati wa mapokezi, Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo amewashukuru madaktari hao kwa kuja nchini kwa kujitolea kuwasaidia wananchi wa Buchosa wenye matatizo mbalimbali ya kiafya, bure.Huduma itaanza kutolewa Jumatatu ya Julai 4, 2022

Shigongo amesema huduma za kitatibu zitaanza Jumatatu ya Julai 4, 2022 na kuwasihi wananchi wenye matatizo mbalimbali, kujitokeza kwa wingi kupata huduma za kitabibu kutoka kwa madaktari hao bure.

Kwa upande wake, kiongozi wa msafara huo, Dk. Bae amesema anajisikia furaha kufika Tanzania ambapo yeye na wenzake wapo tayari kuwapa huduma za kitabibu wananchi waliopo katika visiwa kadhaa vya Ziwa la Victoria pamoja na maeneo mengine na kueleza kwamba wamekuwa na utaratibu wa kuja nchini kila mwaka.

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?

Kampuni Binafsi ziruhusiwe Kuagiza Mafuta Serikali Ipunguze Kodi Kwenye Mafuta.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live