Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madakatari wakutana kujadili ugonjwa wa tezi dume

15599 Tezi+pic TanzaniaWeb

Tue, 4 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Takribani wagonjwa 10 kati ya 60 waliopimwa kwenye kambi maalumu, waligundulika na ugonjwa wa tezi dume licha ya kuwa na afya njema.

Kauli hiyo imetolewa leo Septemba 4, 2018 na Rais wa Chama cha Madaktari wa Hospitali zinazomilikiwa na makanisa (TCMA) Dk Isaya Tosiri alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa siku tatu ulioandaliwa na chama hicho kujadili magonjwa yasiyo ambukiza ikiwamo tezi dume.

Dk Tosiri amesema alipata idadi hiyo ya wagonjwa kutokana na utafiti aliofanya mwaka 2017 ambapo aliweka kambi kwenye Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam.

“Kwenye kambi ile nilipima wagonjwa 60 wenye umri wa miaka 45 na kuendelea ambao walikuwa wazima kabisa, 10 kati yao walibainika na ugonjwa wa tezi dume uliokomaa kabisa licha ya kuendelea na shughuli zao kama kawaida,”amesema Dk Tosiri.

Amesema kutokana na hilo na mapendekezo ya wanachama wengi waliona watumie mkutano huo kujadili kwa kina kuhusu ugonjwa huo na njia watakazochukua kuhakikisha wagonjwa wanapata elimu juu ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

“Elimu kuhusu ugonjwa huu kwa jamii bado ni ndogo na inahitajika nguvu ya pamoja kuhakikisha wananchi wanaelewa.”

“Maeneo mengi wakijadili kuhusu upimaji wa ugonjwa huo, wanajadili mbinu zinazotumika kupima na kuishia kucheka na kuacha kama ilivyo badala ya kuchukua hatua ya upimaji,” amesema.

Amefafanua wao kama hospitali zinazomilikuwa na kanisa ambazo nyingi zipo vijijini watatumia mkutano huo kuwasuka wanachama wao namna ambavyo wataweza kuishawishi jamii ya huko wanakotoa huduma kuona umuhimu wa kupima tezi dume.

Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa TCMA, Dk Bwire Shirangi amezitaja changamoto wanazokutana nao katika utendaji wao kuwa ni pamoja na watumishi wengi kuhamia kwenye hospitali za Serikali.

Amesema hawawezi kuwakataza kwenda huko kwa sababu wanafuata maslahi kama kujiendeleza kielimu, kupanda madaraja na kupata fursa mbalimbali ambazo kwenye hospitali zinazomilikiwa na makanisa hazipatikani.

“Zamani Serikali ilikuwa inaleta watumishi kutoka wizarani wanakuja kuhudumia kwenye hospitali hizi wakipata kila kitu kutoka huko, siku hizi hawaleti na waliopo wanaondoka wakipata nafasi, hivyo tunakuwa na upungufu wa watoa huduma,” amesema Dk Chirangi.

Dk Chirangi amesema jambo lingine linalowavutia watumishi kwenda Serikalini ni kutokana na kupata uhuru.

“Huku kwetu watumishi ni wachache, hivyo hawana uhuru wa kuamua kuondoka muda watakao kwa sababu wakiondoka pengo lao linaonekana moja kwa moja, ”alisema.

Aliitaja changamoto nyingine ni watumishi wengi kukataa kwenda vijijini , hivyo kuongeza uhaba wa wafanyakazi kwenye hospitali na vituo vyao vya afya.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz