Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mabingwa Muhimbili wazungumzia kinachotatiza kwenye Ugumba

Reaywt5er.png Mabingwa Muhimbili wafukua kilichomo katika masamiati ugumba

Thu, 11 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

UNAPOTAJA ugumba, imo katika tatizo linalozikumba jamii nyingi hata kufikia hatua mgogoro na kukatiza uhusiano wao.

Matarajio ya familia nyingi hasa wanandoa, ni kupata watoto muda mfupi baada ya kuonekana ukweli kwamba jambo hilo ni la kibaolojia, imani na lenye kuhitaji subira.

Kitaalamu ugumba unatamkwa kuwa hali ya mwanamke kushindwa kupata ujauzito zaidi ya mwaka mmoja bila ya kutumia njia za kinga za uzazi au mpango wowote. Ni tatizo linalotajwa kuwakumba wenye umri miaka kuanzia 21 hadi 45.

Wanasaikolojia wana maoni dhidi ya dhana potofu kwamba mwanamke pekee ndio chanzo cha kasoro hiyo, ingawa ukweli unamgusa hata mwanamume anayetoa mbegu za uzazi.

MADAKTARI BINGWA

Bingwa wa Magonjwa ya Kinamama na Uzazi kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk. Living Colman, anaiambia Nipashe kwamba tatizo hilo linaongezeka nchini na kati ya wagonjwa 10 anaowaona kwa siku, watatu wana tatizo hilo.

“Kesi za ‘infertility’ ni nyingi sana. Katika kila wagonjwa 10 unaweza kuona watatu au zaidi wenye ‘infertility’. Athari za ugumba hasa ni unyanyapaa kwa wanandoa hasa mwanamke.

“Hali inayoweza kupelekea hata ndoa kuvunjika na kuharibu uhusiano wa jamii kwa pande zote mbili, mume na mke,” anasema bingwa huyo.

Dk. Colman anasema: “Si kweli kwamba matumizi ya dawa za uzazi wa mpango ndio chanzo cha ugumba. Ikiwa zitatumika kwa maelekezo ya mtaalamu, basi husaidia kuzuia mimba kwa muda fulani na pindi unapoziacha, mama anaweza kuendelea kupata ujauzito kama kawaida.

“Kuwapa watoto dawa za uzazi wa mpango ni kuwapa uhuru wa kufanya ngono zembe, hali inayosababisha kupata maambukizi kwenye njia ya uzazi (PID). Hivyo, kuathiri mirija ya uzazi kushindwa kupata ujauzito mbele.”

Dk. Colman anasema ipo haja ya watoto hususan wasichana, kufundishwa kuepuka ngono za mapema zinazochangia maambukizi kwenye mfumo wake wa uzazi na matokeo yake mirija inaziba na kushindwa kushika mimba wakiwa watu wazima, wanapohitaji kuunda familia.

IIi familia iepuke hali hiyo, anasema kuna wajibu wa kutafuta ushauri wa wataalamu wa afya ya kinamama kuhusu afya ya uzazi namna ya kuepuka maambukizi kwenye njia za uzazi, ambayo mirija ya uzazi inaweza kuziba.

SABABU NINI?

Dk. Colman anasema ugumba una vyanzo tofauti na kwamba kwa mwanamke chanzo kikuu ni mayai kushindwa kupevuka kwa mpangilio (hormonal imbalance), ambayo inatokana na hali ya kurithi.

Kadhalika, Dk Colman anasema ulaji vyakula vingi vya sukari na mafuta, unachangia kuwapo unene uliopitiliza na kupungua uzito unaweza kuwa chanzo ugumba.

“Mirija kuziba ndio sababu ya pili ya ugumba kwa mwanamke na hii husababishwa na ngono zembe,” anasema. Kwake mwanamume, sababu ya ugumba inachangiwa na kushindwa kuzalisha mbegu kutokana na mambo kama ulevi wa kupindukia, pia sigara.

“Pia, sababu nyingine ni kuziba mirija ya kupitisha mbegu inayosababishwa na maambukizi,” anafafanua.

TIBA IKOJE?

Dk. Colman anashauri ni vyema kuwaona wataalamu wa afya ambao hufanya vipimo na kugundua tatizo, kisha wanatoa tiba husika.

“Kama ni ‘hormonal imbalance’ atapewa dawa na ushauri na iwapo ni mirija imeziba atashauriwa apandikize’.

“Infertility ipo siku nyingi pengine tangu kuumbwa kwa dunia. Hata kwenye vitabu vya dini tunaona jinsi Nabii Ibrahim na Mkewe Sara walikaa muda mrefu bila ya kupata mtoto. Hata Yohana mbatizaji alipatikana baada ya muujiza.

“Kesi za ugumba ni nyingi sana, Katika kila wagonjwa 10 unaweza kuona watatu au zaidi wenye ‘infertility’. Hakuna jamii ambayo ipo salama na wote wenye uwezo na wasio na uwezo tatizo lipo. umri ni kuanzia miaka 21 mpaka 45,” anasema Dk. Colman.

UZAZI MPANGO

Katika hoja ya dawa za uzazi wa mpango kati ya sababu za tatizo hilo, Dk. Colman anasema si sahihi kwa kuwa matumizi dawa ya uzazi pasipo kuwapo mpangilo mzuri wa watoto katika familia, ingawa anakiri kuwapo matumizi ya dawa isivyo sahihi.

“Ukitizama kwenye jamii hasa mijini, wengi wanatumia njia uzazi wa mpango wa dharura, njia ambayo si sahihi sana, kwani ikitumika kila mara napoteza maana yake.

“Njia nyingine ni kitanzi na kijiti. Hizi ni za muda mrefu na haziingiliani na mfumo wa maisha wa mtu, yaani akishaweka anaendelea na shughuli zake kama kawaida.

‘Kwa uchache watu wanatumia vidonge vya majira na hii ni kwa sababu ya ile hali ya utumwa. Kila siku lazima unywe dawa, inayofanya wengi kuchoka au kusahau na ukisahau kunywa siku moja tu, basi umeharibu dozi nzima,” anafafanua bingwa huyo.

KUPANDIKIZA MIMBA

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Uzazi kutoka MNH, Nathanael Mtinangi, anasema mahitaji ya upandikizaji mimba(In Vitro Fertilisation – IVF) yanaongezeka kila siku nchini, huku hospitali hiyo ikiandaa kituo cha kibingwa cha upandikizaji ikiwamo huduma ya IVF.

Bingwa huyo anasema, hadi sasa wataalamu wake waliopelekwa na MNH masomoni nje ya nchi, walitarajiwa kurejea mwezi uliopita, jengo mashsusi la mradi linaendelea kujengwa na vifaa kuwekwa.

Anasema huduma hiyo itakapoanza nchini, gharama itakuwa nafuu ikilinganishwa na ilivyo sasa. Gharama nje ya nchi ni kati ya Sh. Milioni 15 hadi 40, kutegemea na aina ya huduma, pia tatizo.

MWANASAIKOLOJIA

Mtaalamu wa Saikolojia Tiba, Saldin Kimangale, anasema kwenye jamii watoto wana kinga na usalama kwa ndoa na uhusiano na bila ya wao, wanawake hujihisi hawako salama katika uhusiano.

“Kila mwanamke ana njia zake za kujenga maana juu ya tatizo la ugumba. Wako ambao litawasumbua sana na wako ambao litawasumbua kiasi na wako ambao kwao sio tatizo. Hiyo inategemea rasilimali za ndani alizonazo kiwemo ujasiri, kujiamini, uvumilivu, subira, imani.

“Watoto huwa ni kinga na usalama wa ndoa na mahusiano, bila watoto wanawake hujihisi hawako salama katika uhusiano,: anasema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live