Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maambukizi ya VVU na vifo vimepungua nchini

Vvvvu Upimaji wa VVU waongezeka nchini

Mon, 15 Nov 2021 Chanzo: mwananchidigital

Upimaji wa hiari wa Maambukizi ya virusi vya Ukimwi (VVU) umeongezeka nchini kutoka asilimia 61 mwaka 2016 hadi asilimia 83 mwaka 2019.

Kutokana na mwamko wa upimaji umechangia kupunguza kiwango cha maambukizi mapya katika jamii kutoka asilimia 7 mwaka 2003/2004 hadi asilimia 4.7 mwaka 2016/2017.

Takwimu hizo zimetolewa na Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu, Jenista Mhagama wakati akizungumza kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yanayofanyika kila mwaka Disemba mosi.

Amesema katika kuelekea kuadhimisha miaka 60 ya Uhuru nchi imepiga hatua kubwa pia katika kupunguza vifo vitokanavyo na ugonjwa wa UKIMWI kwa wastani wa asilimia 50 kutoka watu 64000 mwaka 2010 hadi watu 32000 mwaka 2020.

“Kufuatia mafanikio hayo tunajitahidi kuzuia maambukizi mapya ya VVU na tumefanikiwa kupunguza maambukizi hayo kwa watu wazima kwa miaka 15 na zaidi kutoka watu 110,000 mwaka 2010 hadi 68000 mwaka 2020.

Na kwa upande wa maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto yamepungua kutoka asilimia 18 mwaka 2010 hadi asilimia 7 mwaka 2020”amesema.

Hata hivyo licha ya mafanikio hayo Mhagama amesema bado kuna sehemu zimeonekana kuwa na hitaji la kuweka mkazo ili kuendelea kupambana na maambukizi hayo na kufikia lengo la kutokomeza ugonjwa huo ifikapo 2030.

Chanzo: mwananchidigital